-
Walimwengu waandamana kulaani siku 100 za jinai za Israel Gaza
Jan 14, 2024 00:02Mamilioni ya watu jana Jumamosi walifanya maandamano katika pembe mbali mbali za dunia kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na vile vile kuonyesha mshikamano wao na taifa la Palestina.
-
Maandamano ya wananchi wa Uturuki ya kupinga vita
Jan 03, 2024 03:59Katika muendelezo wa maandamano ya kupinga mauaji ya kimbari ya Waislamu huko Gaza, makumi ya maelfu ya wananchi wa Uturuki wamefanya maandamano makubwa mjini Istanbul kupinga jinai za utawala wa Kizayuni na mauaji ya vijana wa Kituruki kaskazini mwa Iraq katika siku ya kwanza ya mwaka huu mpya wa 2024.
-
Waandamanaji Uturuki: Marekani ndiye shetani halisi
Jan 01, 2024 08:25Kwa mara nyingine tena, wananchi wa Uturuki wamekusanyika nje ya Ubalozi Mdogo wa Marekani mjini Istanbul katika maandamano ya kuonyesha himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina hususan wa Ukanda wa Gaza wanaoendelea kukabiliwa na hujuma na mashambulio ya kinyama ya utawala haramu wa Israel.
-
Maelfu washiriki kwenye maandamano ya Morocco ya kuunga mkono Palestina
Dec 25, 2023 03:00Maelfu ya watu nchini Morocco wamefanya mojawapo ya maandamano makubwa zaidi ya kuunga mkono Palestina mjini Rabat, tangu kuzuka kwa vita vya Gaza, wakati wakiitisha kuvunjwa kwa mahusiano kati ya taifa lao na Israel.
-
Watunisia wafanya maandamano makubwa mbele ya ubalozi wa Marekani kuiunga mkono Gaza
Dec 24, 2023 23:11Wananchi wa Tunisia jana Jumapili walifanya maandamano mkabala wa ubalozi wa Marekani katika mij mkuu wa nchi hiyo Tunis, kwa ajili ya kuiunga mkono Gaza. Wananchi wa Tunisia wamekuwa wakiandamana kwa ajili ya kuwaunga mkono raia wa Palestina wa Ukanda wa Gaza na kupinga mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni.
-
Watumishi wa umma Uholanzi waandamana wakitaka kusitishwa vita Gaza
Dec 22, 2023 22:57Makumi ya wafanyakazi wa umma nchini Uholanzi jana Ijumaa waliwashangaza wengi kwa kuingia mabarabarani kushiriki maandamano ya kutaka kutekelezwa usitishaji vita wa kudumu katika Ukanda wa Gaza.
-
Wayemen wafanya maandamano kulaani jinai za Wazayuni Gaza
Dec 15, 2023 06:47Wananchi wa Yemen kwa mara nyingine tena wamefanya maandamano makubwa ya kulaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, na vile vile kuonyesha mshikamano wao na taifa la Palestina.
-
Wacanada waandamana wakimtaka Trudeau aache kuiuzia Israel silaha
Dec 13, 2023 07:45Waungaji mkono wa Palestina wanaoishi nchini Canada wamefanya maandamano makubwa kulaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, ambapo mbali na kuonyesha mshikamano wao na wakazi wa Gaza, lakini pia wamemtaka Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Justin Trudeau kuacha kuuuzia silaha utawala wa Kizayuni.
-
Wanigeria waandamana wakitaka kukatwa uhusiano na Israel
Dec 03, 2023 07:12Kwa mara nyingine tena, maelfu ya Waislamu na waungaji mkono wa Palestina katika mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria wameandamana na kulaani jinai za utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina hasa wa Ukanda wa Gaza.
-
Makumi ya maelfu ya Wamorocco waandamana wakitaka kukatwa uhusiano wa nchi hiyo na Tel Aviv
Nov 28, 2023 01:45Makumi ya maelfu ya wananchi wa Morocco wamefanya maandamano makubwa ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina na kutaka kusitishwa juhudi za kuhuishwa uhusiano kati ya Rabat na Tel Aviv. Wafanya maandamano hao kwa mara nyingine tena wamelaani jinai za utawala haramu wa Israel na kutaka kutekelezwa usitishaji vita wa kudumu huko Ukanda wa Gaza.