Dec 25, 2023 02:41 UTC
  • Watunisia wafanya maandamano makubwa mbele ya ubalozi wa Marekani kuiunga mkono Gaza

Wananchi wa Tunisia jana Jumapili walifanya maandamano mkabala wa ubalozi wa Marekani katika mij mkuu wa nchi hiyo Tunis, kwa ajili ya kuiunga mkono Gaza. Wananchi wa Tunisia wamekuwa wakiandamana kwa ajili ya kuwaunga mkono raia wa Palestina wa Ukanda wa Gaza na kupinga mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni.

Shirika la habari la Farsi limeripoti kuwa, wananchi wengi wa Tunisia jana Jumapili walifanya maandamano makubwa mbele ya ubalozi wa Marekani huko Tunis huku wakipiga nara za kuiunga mkono Palestina na kulaani uungaji mkono wa pande zote wa Marekani kwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhdi ya Gaza. 

Katika maandamano hayo ya jana, wakazi wa mji mkuu wa Tunisia, Tunis walitaka kusitishwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza. Kwa mara kadhaa sasa wananchi wa Tunisia khususan wakazi wa mji mkuu Tunis wanaandamana mbele ya ubalozi wa Marekani mjini humo wakitaka kufukuzwa nchini humo Balozi wa Marekani kutokana na uungaji mkono wa Washington kwa mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza. 

Jinai za utawala wa Kizayuni Ukanda wa Gaza 

Waungaji mkono wa wananchi wa Palestina duniani kote wamekuwa wakifanya maandamano kulaani jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza. 

Wapalestina elfu 20 na 258 wengi wao wakiwa wanawake na watoto wameuliwa shahidi na wengine 53,688 kujeruhiwa tangu kuanza mashambulizi ya utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza. 

Tags