-
Jordan yamzuia balozi wa Israel kurejea mjini Amman
Aug 12, 2017 03:07Serikali ya Jordan imeripotiwa kumzuia balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kurejea mjini Amman hadi pale hatua za kisheria zitakapochukuliwa dhidi ya mlinzi wa ubalozi wa Israel aliyeua raia wawili wa Jordan hivi karibuni.
-
HRW: 27 wauawa katika makabiliano ya polisi na waandamanaji DRC
Aug 11, 2017 02:41Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kwa akali watu 27 waliuawa katika makabiliano baina ya maafisa wa polisi na waandamanaji huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumatatu iliyopita.
-
Wazayuni waandamana kulalamikia ufisadi wa Netanyahu
Aug 06, 2017 02:29Mamia ya Wazayuni wamefanya maandamano katika mji wa Petah Tikva dhidi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu anayeandamwa na tuhuma za ufisadi.
-
Wapinzani waandamana Guinea Conakry juu ya uchaguzi, usalama
Aug 03, 2017 02:49Maelfu ya wafuasi wa kambi ya upinzani huko Guinea Conakry wamefanya maandamano katika mji mkuu Conakry kulalamikia ucheleweshwaji wa uchaguzi sambamba na kuzidi kuwa mbaya hali ya usalama nchini humo.
-
Wairani wafanya maandamano Tehran kulaani jinai za Israel
Jul 28, 2017 21:52Wairani wa matabaka yote jana Ijumaa walifanya maandamano katika mji mkuu Tehran kulaani ukatili unaoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Palestina katika mji mtakatifu wa Quds sambamba na jinai za kutisha dhidi ya Waislamu wa Rohingya.
-
Wairani kufanya maandamano kulaani jinai dhidi ya Wapalestina, Warohingya
Jul 26, 2017 03:34Wairani wa matabaka yote Ijumaa ijayo wanatazamiwa kufanya maandamano ya nchi nzima kulaani ukatili unaoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Palestina katika mji mtakatifu wa Quds na Msikiti wa al Aqsa sambamba na jinai za kutisha dhidi ya Waislamu wa Rohingya.
-
Kuendelea mgogoro na maandamano ya wananchi nchini Morocco
Jul 23, 2017 22:04Katika muendelezo wa machafuko na malalamiko ya wananchi nchini Morocco, askari usalama wa nchi hiyo wamewatia nguvuni makumi ya raia wa nchi hiyo katika mji wa Al Hoceima.
-
Wamorocco waendeleza maandamano Al Hoceima, polisi 72 wajeruhiwa
Jul 22, 2017 11:59Maandamano ya wakazi wa mji wa Al Hoceima, kaskazini mwa Morocco yameendelea huku askari 72 wakijeruhiwa.
-
Wapinzani Madagascar wafanya maandamano licha ya marufuku ya polisi
Jul 08, 2017 12:13Wafuasi wa kambi ya upinzani nchini Madagascar wamefanya maandamano leo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo licha ya maandamano hayo kupigwa marufuku na vyombo vya usalama.
-
Maandamano ya kuunga mkono marekebisho ya katiba ya Mali
Jun 29, 2017 03:04Makumi ya maelfu ya wananchi wa Mali jana waliandamana huko Bamako mji mkuu wa nchi hiyo wakiunga mkono mpango wa kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo.