Wairani wafanya maandamano Tehran kulaani jinai za Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i32404-wairani_wafanya_maandamano_tehran_kulaani_jinai_za_israel
Wairani wa matabaka yote jana Ijumaa walifanya maandamano katika mji mkuu Tehran kulaani ukatili unaoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Palestina katika mji mtakatifu wa Quds sambamba na jinai za kutisha dhidi ya Waislamu wa Rohingya.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 28, 2017 21:52 UTC
  • Wairani wafanya maandamano Tehran kulaani jinai za Israel

Wairani wa matabaka yote jana Ijumaa walifanya maandamano katika mji mkuu Tehran kulaani ukatili unaoendelea kufanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya raia wa Palestina katika mji mtakatifu wa Quds sambamba na jinai za kutisha dhidi ya Waislamu wa Rohingya.

Maandamano hayo yalifanyika baada ya Swala ya Ijumaa ambapo waandamanaji walisikika wakipiga nara zinazosema "Mauti kwa Israel", "Mauti kwa Marekani, Uingereza na Aal-Saud".

Taarifa ya waandamanaji hao imelaani hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kushadidisha jinai zake dhidi ya Wapalestina katika Msikiti wa al-Aqsa, katika mji mtakatifu wa Quds.

Maandamano ya Wairani mjini Tehran

Kadhalika taarifa hiyo ya waandamanaji mjini Tehran imesema kuna haja Waislamu kote duniani kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwao ili kukabiliana na madola ya kibeberu yanayoongozwa na Marekani.

Waandamanaji hao wamewatahadharisha Waislamu dhidi ya kugawanya kwa misingi ya madhehebu zao; harakati zinazoongozwa na magenge ya kigaidi yenye misimamo ya Kiwahabi.

Lengo jingine la maandamano hayo ya Wairani lilikuwa ni kukosoa jinai wanazofanyiwa Waislamu wa Myanmar.

Maafisa usalama wa Israel wakishambulia Wapalestina huko al-Aqsa

Waislamu wa Rohingya nchini Mynanmar zaidi ya elfu moja wameuawa na wengine zaidi ya laki moja kulazimishwa kuwa wakimbizi katika nchi jirani kutokana na ukandamizaji na mauaji ya umwagaji damu yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo ya kufurutu ada wakishirikiana na maafisa usalama wa nchi hiyo tokea mwaka 2012.