-
Waislamu wa Marekani wana hatari ya kunyanyaswa zaidi mwezi wa Ramadhani
May 10, 2018 10:01Baraza la Uhusiano wa Marekani na Uislamu limetaka kuchukuliwa hatua za lazima za kuimarisha usalama kwa ajili ya kuwalinda Waislamu ambao wana hatari ya kukumbwa na mashambulizi na unyanyasaji zaidi katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
-
Kusimama kidete Wapalestina kwawalazimisha Wazayuni kuitisha kikao cha dharura
May 09, 2018 03:20Viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamelazimika kuitisha kikao cha dharura baada ya vyama, mirengo na makundi yote ya Wapalestina kuungana na kusimama imara kukabiliana na uadui wa kupindukia wa rais wa Marekani dhidi ya mji mtakatifu wa Quds wenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu.
-
Shamkhani: Kuvunjika makubaliano ya JCPOA hakutainufaisha Marekani
May 08, 2018 12:33Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesisitiza kuwa kuvunjika kwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA hakutakuwa na manufaa kwa Marekani; na akatoa indhari pia kwa mwenendo wa nchi za Ulaya wa kutaka kujipatia fursa zaidi kwa Jamhuri ya Kiislamu.
-
Wamarekani wengi wanataka US ibakie kwenye JCPOA
May 08, 2018 12:28Utafiti wa maoni wa hivi punde unaonyesha kuwa thuluthi mbili ya wananchi wa Marekani wanaamini kuwa nchi yao haipaswi kujiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran, huku yakiwa yamesalia masaa machache kabla Rais Donald Trump atangaze iwapo Washington itajiondoa kwenye mapatano hayo ya kimataifa au la.
-
Qassemi: Iwapo Marekani itajitoa katika JCPOA, itapata pigo kubwa
May 07, 2018 10:59Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, iwapo Marekani itajitoa katika mapatano ya nyuklia yanayojulikana kwa kifupi kama JCPOA, basi madhara yake yataikumba Washington yenyewe kabla ya upande mwingine wowote.
-
Rais Frank-Walter Steinmeier: Ujerumani tunaunga mkono makubaliano ya JCPOA
May 07, 2018 02:27Rais Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani amesisitiza kuwa, nchi yakke inaunga mkono makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na Iran na pia udharura wa kubakishwa makubaliano hayo.
-
Velayati: Iran itachukua hatua inayofaa endapo Marekani itajiondoa katika makubaliano ya JCPOA
May 06, 2018 22:28Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, endapo Marekani itajiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatoa jibu mwafaka kulingana na mazingira yalivyo.
-
Rahim Safavi: Iran imekwamisha njama na mipango ya Marekani Mashariki ya Kati
May 06, 2018 12:17Msaidizi na Mshauri mwandamizi wa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamuu imekwamisha njama na mipango ya Marekani ya kutaka kuwasha moto na kujikita katika Mashariki ya Kati.
-
Korea Kaskazini: Marekani inachafua anga ya mazungumzo kwa kueneza uwongo
May 06, 2018 03:02Wiki chache kabla ya kufanyika mazungumzo yanayosubiriwa kwa shauku kuu kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, Pyongyang imekosoa vikali kile ilichokitaja kama upotoshaji wa makusudi wa Washington, kwamba sera za Trump za kushadidisha vikwazo na mashinikizo ya kisiasa dhidi ya nchi hiyo ndizo zilizopelekea Korea Kaskazini kukubali kwenda katika meza ya mazungumzo.
-
Shamkhani: JCPOA ni mtihani wa kihistoria kwa ufanisi wa taasisi za kimataifa
May 05, 2018 22:06Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema kudumu au kuvunjika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA, yakiwa ni makubaliano ya kisiasa na kiusalama yaliyothibitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni mtihani wa kihistoria wa kutathmini taathira ya mantiki ya mazungumzo badala ya mizozo na vilevile kiwango cha ufanisi wa taasisi za kimataifa.