• Rwanda yajitetea kuhusu haki za binadamu + Sauti

    Rwanda yajitetea kuhusu haki za binadamu + Sauti

    Feb 08, 2018 04:07

    Serikali ya Rwanda imetangaza kwamba imechukua hatua kubwa ya kuboresha haki za binadamu kwa kutekeleza makubaliano ya kimataifa ya Geneva. Nchi hiyo imetangaza hayo wakati kukiwepo na ukosoaji wa kimataifa kuhusu ukosefu wa uhuru wa kutoa maoni nchini humo. Maelezo zaidi yamo ndani ya ripoti ya mwandishi wetu wa Kigali, Sylvanus Karemera

  • Waziri wa Fedha Uganda matatani + Sauti

    Waziri wa Fedha Uganda matatani + Sauti

    Feb 07, 2018 15:24

    Waziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi wa Uganda anakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka. Maelezo zaidi yamo katika ripoti ya mwandishi wetu wa Kampala, Kigozi Ismail

  • Changamoto za teknolojia barani Afrika + Sauti

    Changamoto za teknolojia barani Afrika + Sauti

    Feb 06, 2018 07:17

    Mataifa ya Afrika yametangaza kuwa yako tayari kushirikiana kuweka sera na sheria moja kuhusu uratibu na matumizi ya teknolojia kwenye medani za kimataifa. Hilo limetangazwa na Muungano wa Kimataifa kuhusu Teknolojia unaojulikana kwa jina maarufu la ITU. Mwandishi wetu wa Kigali na taarifa kamili

  • Changamoto ya wakimbizi Uganda, fedha zatoweka, UN yaingia wasiwasi + Sauti

    Changamoto ya wakimbizi Uganda, fedha zatoweka, UN yaingia wasiwasi + Sauti

    Feb 06, 2018 07:07

    Uganda inakabiliwa na changamoto nyingi kutoka na kuzidi kumiminika wakimbizi nchini humo. Miongoni mwa changamoto hizo ni hitilafu za fedha za kuhudumia wakimbizi zilizoutia wasiwasi Umoja wa Mataifa. Vitambulisho na pasi bandia za kusafiria ni changamoto nyingine. Mwandishi wetu na taarifa zaidi

  • Raila Odinga na kujiapisha kuwa

    Raila Odinga na kujiapisha kuwa "rais wa wananchi wa Kenya" + Sauti

    Jan 31, 2018 03:02

    Raila Odinga, kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Jumanne, Januari 30, 2018 amejiapisha kuwa "rais wa wananchi wa Kenya" katika Bustani ya Uhuru jijini Nairibo kwenye sherehe ambazo licha ya kuhudhuriwa na maelfu ya wafuasi wake, lakini viongozi wenza wa NASA hawakuhudhuria. Mwandishi wa Radio Tehran, Seifullah Murtadha ametuandalia ripoti maalumu kuhusu tukio hilo.

  • Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wazidi kukimbilia Burundi + Sauti

    Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wazidi kukimbilia Burundi + Sauti

    Jan 29, 2018 14:46

    Raia wa eneo la Fizi la mashariki mwa DRC wamekuwa wakikimbia mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi wa Maimai na kukimbilia nchi jirani ya Burundi. Zaidi ya raia elfu 9 wa DRC tayari wamewasili Burundi tangu wiki iliyopita ingawa huduma za kibinadamu za UNHCR hazijaanza kutolewa kwa wakimbizi hao. Mwandishi wetu Hamida Issa na maelezo zaidi.

  • Dk Slaa awataka Watanzania waache ushabiki + Sauti

    Dk Slaa awataka Watanzania waache ushabiki + Sauti

    Jan 29, 2018 14:41

    Watanzania wametakiwa waondoe ushabiki katika masuala muhimu ya maendeleo na siasa ili kuisaidia serikali ifike katika maendeleo ya kweli.

  • Mzanzibari Ali Hilal Ali na msikilizaji wa Radio Tehran Dotto Rangimoto washinda tunzo ya fasihi + Sauti

    Mzanzibari Ali Hilal Ali na msikilizaji wa Radio Tehran Dotto Rangimoto washinda tunzo ya fasihi + Sauti

    Jan 28, 2018 14:33

    Mzanzibari anayejulikana kwa jina la Ali Hilal Ali ameshinda tunzo ya Fasihi ya Kiswahili Afrika kwa mwaka 2017 inayotolewa na Taasisi ya Mabati Cornell yenye makao yake jijini Nairobi Kenya. Taarifa zaidi na mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit.

  • Uganda kuendelea kuunga mkono Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) + Sauti

    Uganda kuendelea kuunga mkono Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) + Sauti

    Jan 27, 2018 04:43

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesisitiza kuwa nchi yake itaendelea kuiunga mkono Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika jitihada zake za kutatua matatizo ya eneo la jumuiya hiyo. Mwandishi wa Radio Tehran mjini Kampala, Kigozi Ismael ametuandalia ripoti hiyo hapo juu

  • Chama cha CUF Tanzania chawakumbuka wanachama wake waliouawa 2001 + Sauti

    Chama cha CUF Tanzania chawakumbuka wanachama wake waliouawa 2001 + Sauti

    Jan 27, 2018 04:39

    Chama cha Wananchi CUF nchini Tanzania kinapeperusha bendera nusu mlingoti kuwakumbuka wanachama wake waliouawa katika maandamano ya mwaka 2001 walipokuwa wanalalamikia kuporwa ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huo, visiwani Zanzibar. Maelezo kamili na mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit.