-
Wakimbizi wa njaa kutoka Somalia wamiminika Kenya
Apr 11, 2017 02:10Ukame ulioathiri sehemu mbalimbali Somalia umesababisha Wasomali wasiopungua 2,000 kuvuka mpaka na kuingia katika kambi ya Dadaab nchini Kenya katika miezi ya hivi karibuni. Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR.
-
Afisa wa serikali Somalia auawa kwenye mlipuko wa bomu Mogadishu
Apr 10, 2017 08:29Afisa wa serikali ya Somalia ameuawa katika mlipuko wa bomu la kutegwa garini huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia. Mlipuko huo umesababisha kifo cha afisa wa ngazi ya chini wa serikali ya Somalia. Hayo yameelezwa na Abdifatah Omar Halane Msemaji wa Meya wa Mogadishu.
-
Watu 15 wauawa katika mlipuko wa bomu Mogadishu, Somalia
Apr 09, 2017 09:52Watu wasiopungua 15 wameuawa baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kuripuka nje ya kambi ya jeshi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
-
Magaidi watano wa Al-Shabab waliohukumiwa kifo Puntland, Somalia wanyongwa
Apr 08, 2017 22:10Eneo la Somalia la Puntland lenye mamlaka yake ya ndani limetekeleza adhabu ya kifo kwa watu watano wanaoaminika kuwa wanamgambo wenye misimamo ya kufurutu mpaka waliohusika na mauaji ya maafisa watatu waandamizi wa serikali ya eneo hilo.
-
Watu watatu wa familia moja wapoteza maisha huko Mogadishu
Apr 07, 2017 09:45Watu wasiopungua watatu wa familia moja wameaga dunia na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia nyumba yao kupigwa na kombora hii leo huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia.
-
UN yatahadharisha kuhusu hatari za maharamia wa Somalia
Apr 05, 2017 22:48Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na mihadarati na uhalifu ametahadharisha kuhusu hatari, vitisho na mashambulizi ya maharamia wa baharini nchini Somalia.
-
Watu kadhaa wauawa katika mripuko wa kigaidi Somalia
Apr 05, 2017 11:40Mripuko wa kigaidi ulioukumba mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, umeua watu kadhaa.
-
Mabaharia kadhaa wa India watekwa nyara katika fukwe za Somalia
Apr 03, 2017 09:52Afisa mmoja anayehusika na vita dhidi ya maharamia wa baharini nchini Somalia ametangaza habari ya kutekwa nyara mabaharia 11 wa India katika fukwe za Somalia.
-
HRW: US kushadidisha hujuma zake za anga Somalia kunahatarisha usalama wa raia
Apr 02, 2017 03:42Hatua ya Marekani ya kuidhinisha kushadidishwa mashambulizi yake ya anga dhidi ya ngome za kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab nchini Somalia imekosolewa vikali na asasi za kutetea za haki za binadamu.
-
UN: Malaki ya raia wa Somalia wamekuwa wakimbizi miezi 4 ya hivi karibuni
Mar 31, 2017 22:29Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, malaki ya watu nchini Somalia wamelazimika kuwa wakimbizi katika miezi minne ya hivi karibuni kutokana na ukame na baa la njaa.