-
Kerry aitaka Sudan Kusini kuheshimu makubaliano ya amani
Aug 23, 2016 03:51Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani amewataka viongozi wa Sudan Kusini kufungamana na makubaliano ya amani ya nchi hiyo.
-
Makamu mpya wa Rais wa Sudan Kusini afanya safari nchini Sudan
Aug 21, 2016 23:27Makamu mpya wa Rais wa Sudan Kusini jana Jumapili alianza safari ya siku mbili ya kuitembelea Sudan ikiwa ni safari yake ya kwanza mjini Khartoum tangu ateuliwe kushika wadhifa huo uliokuwa ukishikiliwa na Riek Machar.
-
UN: Machar yupo salama nchini Kongo DR
Aug 19, 2016 11:55Riek Machar kiongozi wa waasi wa Sudan Kusini na makamu wa zamani wa Rais wa nchi hiyo amekimbilia katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hayo yameelezwa na Umoja wa Mataifa.
-
Kenya yatathmini kutuma wanajeshi Sudan Kusini
Aug 18, 2016 22:22Bunge la Kenya linatazamiwa kujadili hoja ya iwapo serikali ya Nairobi itatuma wanajeshi wa nchi hiyo KDF nchini Sudan Kusini au la, wiki moja baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupasisha azimio la kutumwa askari 4,000 zaidi nchini humo.
-
Dak: Machar ametoroka Sudan Kusini kwa kuandamwa na maafisa usalama
Aug 18, 2016 09:25Msemaji wa kiongozi wa upinzani nchini Sudan Kusini amesema Riek Machar ameikimbia nchi hiyo kutokana na kuandamwa na maafisa usalama wa serikali, ambao wamekuwa wakimsaka kwa udi na uvumba tangu aukimbie mji mkuu Juba zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
-
Deng Gai: Machar ndiye anayekwamisha mchakato wa amani S/Kusini
Aug 17, 2016 09:25Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan Kusini, Taban Deng Gai amemlaumu mtangulizi wake katika kiti hicho Riek Machar aliyeutoroka mji wa Juba kuwa amevuruga mchakato wa amani na kukiuka makubaliano ya kusitisha machafuko ya miezi kadhaa katika nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.
-
UN kuchunguza radiamali ya walinda amani kufuatia kushambuliwa hoteli moja S/Kusini
Aug 17, 2016 03:14Ban Ki-moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameanzisha uchunguzi kuhusu tuhuma zinazowakabili askari jeshi wa kulinda amani huko Sudan Kusini (UNMISS) kwamba walishindwa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na shambulio la watu wenye silaha dhidi ya hoteli moja huko Juba.
-
Rais Kiir: Askari wa nchi za Afrika wataanza kuwekwa katika mipaka ya Sudan na Sudan Kusini
Aug 15, 2016 23:24Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesema kuwa, nchi yake imejiandaa kwa ajili ya kuwekwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika katika mipaka ya pamoja na nchi ya Sudan.
-
Kiir akataa azimio la kutumwa askari 4,000 zaidi Sudan Kusini
Aug 14, 2016 03:10Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amekataa azimio lililopasishwa Ijumaa iliyopita na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutumwa askari 4,000 zaidi wa kigeni nchini humo.
-
Pendekezo la Marekani kushadidisha mgogoro wa kisiasa nchini Sudan Kusini
Aug 12, 2016 10:40Imeelezwa kuwa utekelezwaji wa pendekezo la Marekani nchini Sudan Kusini utashadidisha mgogoro wa kisiasa wa taifa hilo changa zaidi barani Afrika.