Pendekezo la Marekani kushadidisha mgogoro wa kisiasa nchini Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i13129-pendekezo_la_marekani_kushadidisha_mgogoro_wa_kisiasa_nchini_sudan_kusini
Imeelezwa kuwa utekelezwaji wa pendekezo la Marekani nchini Sudan Kusini utashadidisha mgogoro wa kisiasa wa taifa hilo changa zaidi barani Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 12, 2016 10:40 UTC
  • Pendekezo la Marekani kushadidisha mgogoro wa kisiasa nchini Sudan Kusini

Imeelezwa kuwa utekelezwaji wa pendekezo la Marekani nchini Sudan Kusini utashadidisha mgogoro wa kisiasa wa taifa hilo changa zaidi barani Afrika.

Ripoti iliyotolewa leo Ijumaa imeeleza kwamba, pendekezo la serikali ya Washington katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kutumwa askari 4,000 nchini Sudan Kusini, litashadidisha maradufu mgogoro wa nchi hiyo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo pendekezo hilo la Marekani linasisitizia kutumwa askari hao wa kieneo kwa ajili ya kutekeleza operesheni za kijeshi ndani ya ardhi ya nchi hiyo.

Mapigano makali Sudan Kusini

Katika sehemu nyingine ya azimio hilo ambalo lilisambazwa kwa wajumbe 15 wa Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa, imeelezwa kuwa endapo serikali ya Juba haitoafikiana nalo na likakubaliwa na Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa umoja huo, hatua hiyo itaandaa mazingira ya kupitishwa vikwazo vya silaha dhidi ya Sudan Kusini ndani ya umoja huo. Machafuko na mgogoro wa kisiasa nchini Sudan Kusini ulizuka mwezi Disemba mwaka 2013, baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake wa rais Riek Machar kuwa alikuwa amepanga njama za kumpindua.

Hali mbaya ya kibinaadamu nchini Sudan Kusini