Idadi ya mashahidi wa Palestina huko Gaza yafikia 2700
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103562-idadi_ya_mashahidi_wa_palestina_huko_gaza_yafikia_2700
Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza ongezeko la idadi ya mashahidi na waliojeruhiwa katika hujuma ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 16, 2023 10:19 UTC
  • Idadi ya mashahidi wa Palestina huko Gaza yafikia 2700

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza ongezeko la idadi ya mashahidi na waliojeruhiwa katika hujuma ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa Kanali ya Televisheni ya Al-Mayadeen, Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, idadi ya mashahidi wa Kipalestina wakati wa mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza imeongezeka na kufikia 2,750.

Kwa mujibu wa tangazo la wizara hii, zaidi ya Wapalestina 9,700 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo ya kinyama ya adui Mzayuni katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Ghaza.

Kadhalika, tangu kuanza hujuma za utawala wa Kizayuni, Wapalestina 58 wameuawa shahidi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na wengine 1,250 wamejeruhiwa.

 

Jana usiku, timu za misaada za Gaza vilitangaza kuwa zaidi ya watu 1,000 wamezikwa chini ya vifusi vya nyumba zilizoharibiwa. Timu za misaada zinaeleza kuwa, baadhi ya watu walioachwa chini ya vifusi wametoka hai saa 24 baada ya mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni.

Timu za misaada zinaonya kuwa, kuendelea kwa uvamizi dhidi ya Gaza kutasababisha maafa ya kweli na kutatufanya tushindwe kutekeleza majukumu yetu kwa taifa letu.

Mfuko wa Idadi ya Watu wa Umoja wa Mataifa pia umetangaza kuwa, zaidi ya wanawake 50,000 wajawazito katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na hali ya janga karibu wakati huuu wa kukkaribia kusambaratika kabisa kwa mfumo wa afya katika eneo hilo.

Kulingana na ripoti hiyo, inatabiriwa kuwa takriban watoto 5,000 watazaliwa mwezi ujao katika hali ngumu sana na isiyofikirika.