Hamas, Jihad Islami zaapa: Mapambano dhidi ya Israel yatapamba moto zaidi
(last modified 2024-08-03T04:29:16+00:00 )
Aug 03, 2024 04:29 UTC
  • Hamas, Jihad Islami zaapa: Mapambano dhidi ya Israel yatapamba moto zaidi

Makundi ya Muqawama na mapambano ya ukombozi wa Palestina yenye makao yao huko Gaza, Hamas na Jihad Islami yamesisitiza kuwa, mauaji yanayofanywa na Israel dhidi ya viongozi wa kambi ya Muqawama hayatadhoofisha nguvu ya mapambano dhidi ya utawala huo ghasibu.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Hamas na Jihad Islami imesema: Muqawama na mapambano ya ukombozi ni haki halali kwa ajili ya kukabiliana na uvamizi, na mapambano hayo yataendelea hadi watu wa Palestina watakapopata haki zao zote na kurudi katika nchi yao.

Taarifa hiyo imewata wananchi wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na maeneo mengine yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina kuzidisha mapambano na kuzima mipango ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Hamas na Jihad Islami zimesisitiza kuwa: "Israel haijapata na haitafikia malengo yake katika vita isipokuwa kuua na kufanya uharibifu, na hili halitatuzuia mapambano ya ukombozi; na tutaendelea na kazi yetu ya pamoja na uratibu endelevu katika ngazi za kisiasa, kijeshi na nyanjani."

Image Caption

"Muqawama unamuahidi Mwenyezi Mungu kwanza, na kisha watu wetu na taifa letu, kwamba utatekeleza wajibu wake wa kutetea watu wetu, ardhi yetu, kulinda matakatifu yetu, na kulinda haki zetu halali, kwa gharama yoyote ile", imesisitiza taarifa hiyo."

Israel ilianzisha mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Gaza tarehe 7 Oktoba mwaka jana na hadi sasa imeua karibu Wapalestina elfu 40, wengi wao wakiwa wanawake na watoto wadogo. 

Tags