Aug 28, 2024 15:20 UTC
  • Wapalestina waliouawa shahidi Gaza wakaribia 50,000

Idadi ya mashahidi wa vita vya mauaji ya halaiki huko Gaza yanauyotekelezwa na utawala haramu wa Israel imekaribia 50,000.

Ripoti kutoka Palestina zinasema kuwa, Wapalestina wengine 58 wameuawa shahidi na kufanya idadi ya mashahidi wa Palestina walioawa shahidi huko Gaza tangu kuanza kwa hujuma ya kinyama ya Israel Oktoba mwaka jana (2023) kufikia 40,534.

Wakati huo huo, Uchunguzi wa hivi karibuni kabisa wa Shirika la Kimataifa la Amnesty International unaonesha kuwa, utawala wa Kizayuni umefanya jinai za kutisha na unaendelea kukanyaga kikamilifu sheria na mikataba wa kimataifa.

Sehemu moja ya tamko la Amnesty International imesema: Utawala wa Israel umetumia silaha zilizopigwa marufuku kwenye mashambulio yake ya anga dhidi ya kambi ya wakimbizi huko Rafah na maeneo mengine yenye mrundikano wa raia ya Ukanda wa Ghaza.

Hujuma na mashambulio ya kinyama ya Israel yanavyoendelea kuharibu makazi ya watuu huko Gaza

 

Zaidi ya miezi 10 imepita hivi sasa tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha jinai za pande zote dhidi ya wananchi wa Ghaza huko Palestina, lakini umeshindwa kufikia malengo yake, zaidi ya kufanya jinai za kutisha za kuua kwa umati wanawake, watoto wadogo na raia wa kawaida.

Kwa upande mwingine, licha ya kwamba Israel inachuja mno habari, lakini jeshi la utawala huo dhalimu juzi lililazimika kutangaza kuangamizwa mmoja wa afisa wa ngazi za juu wa jeshi lake kutoka brigedi ya 9207 na kukiri kwamba hadi hivi sasa wanajeshi 702 wa Israel wameshaangamizwa katika vita vya Ghaza. Siku tano nyuma pia, utawala wa Kizayuni ulikiri kuangamizwa wanajeshi wengine kadhaa wa Israel huko Ghaza.

Tags