Jul 21, 2016 08:05 UTC

Magaidi wa Syria wa kundi la Nuruddin al Zanki wanaoungwa mkono na madola ya kieneo na ya Magharibi hasa Marekani, yamezidi kudhihirisha ukatili wao kwa kumchinja kama kuku mtoto mdogo wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 12.

Licha ya mtoto huyo kuwa na maradhi ya talasemia unaohitajia kubadilishwa damu mara kwa mara, lakini magaidi haio hata hawakumuhurumia. Bali kwa kejeli walimuuliza aseme matumaini yake ya mwisho kabla yawajamchinja. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba mtoto huyo aliwaomba magaidi hao wamuue kwa kumpiga risasi, wasimchinje, lakini wapi!!! 

Tags