Duru ya Kizayuni: Netanyahu anajaribu kuvuruga makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza
(last modified Mon, 10 Feb 2025 02:42:17 GMT )
Feb 10, 2025 02:42 UTC
  • Duru ya Kizayuni: Netanyahu anajaribu kuvuruga makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza

Chombo kimoja cha bahari cha lugha ya Kiibrania kimetangaza kuwa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel anafanya kila awezalo kuvuruga makubaliano ya kusimamisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.

Gazeti la Haaretz limevinukuu vyanzo vya Kizayuni na kuandika: Netanyahu yumkini akasambaratisha makubaliano ya kubalishana mateka kati ya utawala wa kizayuni na harakati ya Hamas. 

Haaretz limeongeza kuwa: Timu iliyosafiri hadi Doha mji mkuu wa Qatar imesema kuwa haitajaribu kuendeleza awamu ya pili ya makubaliano hayo, na kwamba Netanyahu ametangaza kuwa hataki kuyatekeleza. Limeongeza kuwa, Netanyahu ametuma timu ya mazungumzo yenye ushawishi mdogo na haina uwezo wa kuchukua hatua yoyote ya kivitendo.

Duru hiyo ya habari ya Kizayuni imeendelea kubainisha: Netanyahu anaamini kuwa picha za wakati wa kuachiliwa huru mateka wa utawala wa Kizayuni huko Gaza zilikuwa na taathira hasi katika uchunguzi wa maoni wa fikra za waliowengi. 

Duri hiyo ya habari ya Haaretz imesema kuwa, picha na mabango ya kejeli yaliyowekwa na Brigedi za al-Qassam kuhusu "ushindi kamili" yamemfanya Netanyahu aamini kuhusu uwezekano wa kupoteza baraza lake la mawaziri ikiwa hatokamilisha mpango huo.