Kuendelea mashambulizi na jinai za Wazayuni kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi
wanajeshi wa utawala wa Kizayuni kwa mara nyingine tena wameshambulia maeneo mbalimbali katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Jeshi la utawala wa Kizayuni jana alasiri liliharibu na kubomoa miundomsingi ya makazi ya raia katika maeneo ya Qabatiyeh na Berkini katika mji wa Jenin kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kwa kutumia mabuldoza yakijeshi.
Katika hujuma yao hiyo, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni walizifunga njia na barabara zinazoelekea katika maeneo ya Qabatiyeh na Berkin na kubomoa barabara, miundombinu ya maji na umeme na kuharibu mali mbalimbali katika maeneo hayo.
Watu walioshuhudia wameeleza kuwa, jeshi la utawala wa Kizayuni lilivamia nyumba kadhaa za raia wa Palestina na kuwatia nguvuni watu kadhaa.
Jana alasiri pia ndege zisizo na rubani za jeshi la Israel ziliruka katika anga ya mji wa Jenin katika Ukingo wa Magharibi na katika maeneo ya kandokando ya mji huo ili kufuatilia harakati za Wapalestina.
Makundi mbalimbali ya Palestina yameonya kuwa kuendelea mshambulizi ya jeshi la Israel katika Ukingo wa Magharibi kutakabiliwa na jibu kali na la wazi la muqawama.