Mipapurano Israel, mkuu wa ujasusi nje! Haaretz: Netanyahu atupeleka kuzimu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i124040-mipapurano_israel_mkuu_wa_ujasusi_nje!_haaretz_netanyahu_atupeleka_kuzimu
Hatua ya waziri mkuu wa Israel ya kutangaza kumfuta kazi mkuu wa genge la kijasusi la Shin Bet la utawala wa Kizayuni kwa madai kuwa hana imani naye, imeleta tetemeko jingine kubwa ndani ya utawala huo pandikizi.
(last modified 2025-03-17T22:42:05+00:00 )
Mar 17, 2025 22:42 UTC
  • Mipapurano Israel, mkuu wa ujasusi nje! Haaretz: Netanyahu atupeleka kuzimu

Hatua ya waziri mkuu wa Israel ya kutangaza kumfuta kazi mkuu wa genge la kijasusi la Shin Bet la utawala wa Kizayuni kwa madai kuwa hana imani naye, imeleta tetemeko jingine kubwa ndani ya utawala huo pandikizi.

Gazeti la Haaretz la utawala wa Kizayuni limeandika katika tahariri ya toleo lake la jana Jumatatu kwamba, waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu anaupeleka kuzimu utawala wa Kizayuni kwa hatua yake ya kumfuta kazi Ronen Bar, mkuu wa genge la kijasusi la Israel, Shin Bet. Gazeti hilo limeandika: "Kama Netanyahu ataendelea kushika lijamu ya siasa, basi Israel itapata hasara kubwa isiyofidika."

Hayo yamekuja baada ya mahakama moja ya Israel kuzuia kusambazwa taarifa za kesi ambayo genge la kijasusi la utawala wa Kizayuni la Shin Bet linaifuatilia kuhusu afisa mmoja wa ngazi za juu wa ofisi ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu.

Gazeti la Kizayuni la Haaretz linashinikiza kutangazwa taarifa za afisa huyo wa ngazi za juu wa karibu na Netanyahu, lakini halikusema afisa huyo anakabiliwa na mashitaka gani.

Kwa upande wake, Kanali ya 13 ya Televisheni ya Israel imefichua kuwa, makachero wa utawala wa Kizayuni wanafuatilia kesi ya uwezekano wa Qatar kuwapa watu wa karibu na waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, mamia ya maelfu ya dola na wanataka kujua fedha hizo zimekwenda wapi.

Televisheni hiyo ya Israel imeendelea kufichua kwamba, watu wa karibu na Netanyahu walihongwa mamia ya maelfu ya dola na Qatar ili kusaidia kusafisha sura ya waziri mkuu huyo wa Israel kabla ya Qatar kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia za Mpira wa Miguu mwaka 2022.