UN yataka kila mwenye ushawishi azuie mashambulizi ya Israel huko Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i124070-un_yataka_kila_mwenye_ushawishi_azuie_mashambulizi_ya_israel_huko_ghaza
Tom Fletcher, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu ameonesha hisia zake kuhusu taarifa za kutisha za mashambulizi mabaya ya Israel dhidi ya Ghaza, akisema kuwa, kila mwenye ushawishi ana wajibu wa kufanya kadiri awezavyo kukomesha jambo hilo.
(last modified 2025-03-18T08:00:00+00:00 )
Mar 18, 2025 08:00 UTC
  • UN yataka kila mwenye ushawishi azuie mashambulizi ya Israel huko Ghaza

Tom Fletcher, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu ameonesha hisia zake kuhusu taarifa za kutisha za mashambulizi mabaya ya Israel dhidi ya Ghaza, akisema kuwa, kila mwenye ushawishi ana wajibu wa kufanya kadiri awezavyo kukomesha jambo hilo.

Fletcher ameandika hayo kwenye mtandao wa kijamii wa X na kusema: "Wasaidizi wetu wa masuala ya kibinadamu wamefanya kila linalowezekana kuokoa maisha ya watu wengi kadiri tunavyoweza huko Ghaza. Kila mtu aliye na ushawishi lazima asitishe jambo hili."

Nazo familia za mateka wa Kizayuni walioko mikononi mwa makundi ya Muqawama wa Palestina zimetaka kufanyike maandamano makubwa ya kulaani jinai mpya za utawala wa Kizayuni kwenye Ukanda wa Ghaza zikisema kuwa, jamaa zao wako hatarini kutokana na mashambulizi hayo mapya ya Israel. 

Taarifa ya pamoja ya familia hizo imesema: "Hakuna jambo la haraka zaidi kuliko hili! Mashambulizi ya kijeshi yatasababisha kuuawa mateka walio hai na kutopatikana kabisa miili ya waliouawa!"

Kwa upande wake, Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) lenye makao yake makuu mjini Washington, DC, limeilaani serikali ya Netanyahu kwa kuanzisha wimbi jipya la jinai, mashambulizi ya kutisha na mauaji ya kimbari dhidi ya wanaume, wanawake na watoto wa Ghaza na kuua mamia ya raia wasio na hatia katika muda wa saa chache tu.

Taarifa ya CAIR imesema: "Netanyahu yuko tayari kuua watoto wote wa Palestina katika kambi za wakimbizi kuliko kukabiliana na hatari ya kusambaratika serikali yake kupitia kubadilishana mateka wanaoshikiliwa na pande zote mbili na kumaliza kabisa vita na mauaji ya kimbari, kama inavyotakiwa na makubaliano ya kusitisha mapigano."