Zainab Nasrullah: Kuwauwa viongozi wa Muqawama hakutadhoofisha mapambano
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i124474-zainab_nasrullah_kuwauwa_viongozi_wa_muqawama_hakutadhoofisha_mapambano
Binti wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa kuwauwa viongozi wa Muqawama hakutadhoofisha mapambano ya ukombozi.
(last modified 2026-06-22T10:26:06+00:00 )
Mar 28, 2025 08:40 UTC
  • Zainab Nasrullah
    Zainab Nasrullah

Binti wa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, aliyekuwa Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa kuwauwa viongozi wa Muqawama hakutadhoofisha mapambano ya ukombozi.

Zainab Nasrullah, ambaye alikuwa akizungumza leo kabla ya hotuba ya Swala ya Ijumaa ya mjini Tehran amesema mbele ya umati wa watu waliohudhuria ibada hiyo sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwamba: Tunaahidi mbele ya Mwenyezi Mungu, Imam wetu wa Zama, marehemu Imam Khomeini (M.A) na shahidi wetu Sayyid Hassan Nasrullah, kwamba tutaendeleza njia ya Muqawama na kuikamilisha njia hii, hata kama sisi sote tutakufa shahidi. 

Binti wa Katibu wa zamani Hizbullah ya Lebanon ameashiria matamshi ya Sayyid Hassan Nasrullah na kusema: Sayyid shahidi wetu mara kadhaa alitilia mkazo nukta kwamba "Lebanon haitakuwa katika mikono ya Israel abadani", kwa hiyo msidanganywe na kumwagwa damu zetu, kwa sababu damu hizi daima zimekuwa washindi na zitaendelea kushinda siku zote; Na tunaamini ahadi na nusra ya Mwenyezi Mungu."