Kushadidi maandamano na malalamiko ya kisiasa huko Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i124484-kushadidi_maandamano_na_malalamiko_ya_kisiasa_huko_israel
Huku maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yakifanyika katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kuunga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel, mivutano ya kisiasa na hitilafu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu nayo imeongezeka na kupamba moto zaidi.
(last modified 2025-03-28T22:59:10+00:00 )
Mar 28, 2025 22:59 UTC
  • Kushadidi maandamano na malalamiko ya kisiasa huko Israel

Huku maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yakifanyika katika nchi mbalimbali kwa ajili ya kuunga mkono Palestina na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel, mivutano ya kisiasa na hitilafu katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu nayo imeongezeka na kupamba moto zaidi.

Jana ilikuwa Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na Siku ya Kimataifa ya Quds. Wananchi wa Iran na nchi mbalimbali duniani walifanya maandamano makubwa ya kueleza uungaji mkono wao kwa mapambano ya ukombozi ya Wapalestina na kulaani jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza. Ndani ya maeneo yanayokaliwa kwa mabavu, mivutano ya kisiasa imeongezeka, na maandamano dhidi ya baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu yanapamba moto siku baada ya siku.

Kwa upande wa kisiasa, utawala ghasibu wa Israel unashuhudia ongezeko kubwa la mivutano kutokana na mzozo unaoongezeka kati ya baraza la mawaziri la Benjamin Netanyahu, mahakama na Idara ya Usalama wa Ndani (Shin Bet). Hitilafu na mizozo imeshadidi zaidi ndani ya utawala ghasibu wa Israel kutokana na uamuzi wa Netanyahu wa kumfukuza kazi Ronen Bar, aliyekuuwa mkuu wa Huduma ya Usalama wa Ndani (Shin Bet), na baadaye zuio la muda na Mahakama ya Juu ya Israel la kusitisha uamuzi huo.

Maandamano dhidi ya serikali ya Netanyahu, Tel Aviv

Netanyahu pia alimfukuza kazi mshauri wa masuala ya mahakama wa baraza la mawaziri, Baharav-Miara. Kwa hivyo, tofauti kati ya baraza la mawaziri, vyombo vya usalama, na mshauri wa mahakama wa baraza la mawaziri zimepelekea kutokota zaidi mivutano ya kisiasa ndani ya utawala wa kibaguzi wa Israel. Kambi ya upinzani na wachambuzi wanaiona hatua ya Netanyahu ya kumfukuza mshauri wa masuala ya mahakama wa baraza la mawaziri kama sehemu ya jitihadi zake na kundi la wanasiasa wenye siasa kali za kidini za kutaka kudhibiti mahakama na taasisi nyingine kadhaa muhimu.

Nia ya kutaka kudhibiti Idara ya Mahakama ilikuwepo tangu mwanzoni kabisa mwa uwaziri mkuu wa Benjamin Netanyahu mnamo Januari 2022, suala ambalo lilisababisha maandamano makubwa zaidi ya umma dhidi ya baraza la mawaziri la Netanyahu. Wakosoaji na umma, wanaona kuwa sasa, Netanyahu ameanza jitihada mpya za kujaribu kudhibiti Idara ya Mahakama na kuzidisha mamlaka yake.

Hitilafu hizi, pamoja na kuanza tena vita dhidi ya watu wa Gaza na kushindwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas, vimekuwa chachu ya duru mpya ya maandamano ya wananchi dhidi ya baraza la mawaziri la Netanyahu. Makumi kwa maelfu ya watu wameingia mitaani katika siku za hivi karibuni kupinga sera za Netanyahu, ambazo wanazielezea kuwa zinatishia "misingi na kanusi za kidemokrasia."

Kufeli makubaliano ya usitishaji vita na kuhatarisha maisha ya mateka wa Kizayuni waliosalia mikononi mwa wapigania ukombozi wa Kipalestina ni sababu nyingine ya maandamano ya makumi ya maelfu ya watu dhidi ya utawala wa Israel. Hassan Nafea, profesa wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Cairo, anasema, "kesi ya mateka wa Israel wanaoshikiliwa huko Gaza imekuwa suala lilalozusha mjadala na mvutano mkubwa. Mizozo ya ndani na kutoweza serikali kushughulikia kesi hii kumepelekea kuanzishwa tena maandamano huko Israel."

Alaa kulli hal, maoni ya umma ya kimataifa pia jana katika Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani yalionyesha kuchukizwa kwake na utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendelea kufanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina husuusan wanawake na watoto wa Gaza. Kwa kuzingatia hali hiyo, tunaweza kusema kuwa, licha ya himaya na uungaji mkono endelevu wa Wamagharibi kwa Israel, lakini utawala huo unakabiliwa na changamoto nyingi zaidi za ndani na nje kuliko hapo awali.