Kwa nini mashambulizi ya Marekani dhidi ya Wayemen hayana athari?
Kanali ya 12 ya Televisheni ya Utawala wa Kizayuni imekiri kuwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya Yemen hayajazaa matunda. Licha ya mashambulizi hayo kuongezeka, hayakuweza kuzuia mashambulizi ya makombora yanayoelekezwa Israel.
Je, ni dalili gani zinazothibitisha kuwa mashambulizi ya Marekani dhidi ya Yemen hayana athari?
Mashambulizi ya Majeshi ya Yemen dhidi ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, ambazo zimepacikwa jina bandia la 'Israel', bado yanaendelea. Jumapili iliyopita, kombora lililorushwa kutoka Yemen liliwalazimisha mamilioni ya Wazayuni kukimbilia kwenye maeneo ya kujificha chini ya ardhi.
Pia, msemaji wa jeshi la Yemen, Jenerali Yahya Saree, amesema katika siku za hivi karibuni wanajeshi wa Yemen walishambulia mara kadhaa meli ya kivita ya Marekani yenye uwezo wa kusheheni ndege za kivita, USS Harry Truman, pamoja na meli nyingine za kijeshi katika Bahari Nyekundu. Alisema operesheni hizi zinaonyesha kuwa Marekani imeshindwa kuzima uwezo wa Yemen kusaidia watu wa Palestina.
Swali muhimu linabaki: Kwa nini mashambulizi ya Marekani hayana athari?
Kwanza, Marekani haijaelewa vizuri utamaduni wa kisiasa wa Yemen. Historia inaonyesha kuwa Wayemen hawakubali kutishwa wala kushinikizwa. Vita vya miaka 8 vya Saudi Arabia dhidi ya Yemen ni ushahidi wa uvumilivu huo.
Pili, mashambulizi ya Yemen yamejikita katika imani ya kidini, ambayo Marekani haielewi vizuri. Wanafikiri kwa mabomu wanaweza kuzima imani ya Kiislamu, lakini hawajui kuwa imani hiyo ndiyo nguvu ya mashambulizi hayo.
Tatu, harakati ya Ansarullah inaungwa mkono sana na wananchi. Maandamano ya mamilioni ya watu kufuatia mwito wa viongozi wao ni dalili ya nguvu hiyo ya kijamii.
Kwa hivyo, mashambulizi ya karibu kila siku ya Marekani dhidi ya Yemen hayawezi kuwazuia Wayemen katika azma yao ya kujitetea na kuwanga mkono Wapalestina wanakandamizwa na Israe – bali yanazidi kuipa nguvu nchi hiyo ya Kiarabu.