Al-Qassam yamwangamiza askari wa Kizayuni baada ya kutofanikiwa kumkamata mateka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128156-al_qassam_yamwangamiza_askari_wa_kizayuni_baada_ya_kutofanikiwa_kumkamata_mateka
Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS limetangaza kuwa limelazimika kumuangamiza mwanajeshi mmoja wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Ghaza baada ya mazingira kwenye medani ya mapambano kutoruhusu kumkamata mateka.
(last modified 2025-07-10T09:42:34+00:00 )
Jul 10, 2025 09:40 UTC
  • Al-Qassam yamwangamiza askari wa Kizayuni baada ya kutofanikiwa kumkamata mateka

Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS limetangaza kuwa limelazimika kumuangamiza mwanajeshi mmoja wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Ghaza baada ya mazingira kwenye medani ya mapambano kutoruhusu kumkamata mateka.

Utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri kuwa askari wake mmoja ameuawa katika operesheni hiyo.

Hilo ni tukio la kwanza la aina hiyo katika kipindi cha miezi 14 ikiwa ni sehemu ya operesheni kali zinazofanywa na makundi ya Muqawama ya Wapalestina katika kukabiliana na mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na utawala bandia wa Israel katika Ukanda wa Ghaza.

Tangu utawala wa Kizayuni ulipoanzisha tena mashambulizi yake ya kinyama huko Ghaza tarehe 18 Machi, wanajeshi wake 39 wameangamizwa na Wanamuqawama wa Muqawama katika Ukanda huo.

Hayo ni kwa mujibu wa gazeti la kila siku la lugha ya Kiebrania la Israel Hayom.

Taarifa iliyotolewa na Al-Qassam imesema: "tulifanya shambulio kwenye mkusanyiko wa askari wa adui na magari yao katika eneo la Abasan al-Kabira, mashariki mwa Khan Younis."

Tawi hilo la kijeshi la Hamas limebainisha kuwa wapiganaji wake walikilenga kifaru cha Merkava, shehena ya kubeba askari wenye silaha, na tingatinga mbili za kijeshi kwa kutumia makombora ya Al Yassin 105.

"Wapiganaji wetu walisonga mbele kuelekea walipokuwa askari wa adui na wakapambana nao kwa kutumia silaha nyepesi. Walijaribu kumkamata askari mmoja, lakini hali kwenye medani haikuruhusu, hivyo wakamuua na kukamata silaha yake".../