Raia 33 wa Yemen wauawa katika hujuma ya anga ya Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i12931-raia_33_wa_yemen_wauawa_katika_hujuma_ya_anga_ya_saudia
Kwa mara nyingine tena ndege za kijeshi za Saudi Arabia zimeshambulia maeneo ya makazi ya watu na kuua makumi ya raia wasio na hatia katika mikoa kadhaa ya Yemen hii leo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 09, 2016 08:45 UTC
  • Raia 33 wa Yemen wauawa katika hujuma ya anga ya Saudia

Kwa mara nyingine tena ndege za kijeshi za Saudi Arabia zimeshambulia maeneo ya makazi ya watu na kuua makumi ya raia wasio na hatia katika mikoa kadhaa ya Yemen hii leo.

Kanali ya televisheni ya al-Masira ya Yemen imeripoti kuwa, watu zaidi ya 33 wameuawa katika mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na ndege za utawala wa Aal-Saud leo Jumanne katika maeneo ya Qatabir, Sana'a, mkoa wa Hajjah, wilaya ya Kushar, mikoa ya Sa’ada na Ibb na wilaya za Saqayn na Sahar.

Shambulio la anga la Saudia dhidi ya jengo la makazi ya raia Yemen

Aidha ndege hizo zimeshambulia kwa mabomu vituo vya kijeshi vya al-Sama katika wilaya ya Arhab na Hamza katika mkoa wa Ibb.

Mapema siku ya Jumapili ndege za kivita za vikosi vamizi vya Saudia ziliua watu wasiopungua 14 katika shambulio la anga dhidi ya mji mkuu wa Yemen, Sana'a.

Mashambulizi ya anga ya jeshi la utawala  wa Aal-Saud tokea Machi mwaka jana hadi sasa yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 10,000 nchini Yemen. Kwa mujibu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen, Saudi Arabia imeua watoto karibu 2,000 wa Yemen na kuvunja haki za maelfu ya wengine katika hujuma zake hizo.

Watoto ndio wahanga wakuu wa hujuma za Saudia nchini Yemen

Jana Jumatatu, Baraza la Wakimbizi la Norway lilionya kuwa, Yemen imetumbukia katika mgogoro mkubwa wa wakimbizi katika muda wa siku 500 za hujuma za ndege za Riyadh na kwamba inaelekea kuwa tatizo hilo la wakimbizi litashindikana kutatuliwa.