Balozi Mzayuni asababisha kufutwa mkutano Afrika Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1441-balozi_mzayuni_asababisha_kufutwa_mkutano_afrika_kusini
Mkutano uliokuwa ufanyike mjini Johannesburg, kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro wa maji nchini Afrika Kusini umefutwa kutokana na kulalamikiwa vikali kualikwa balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye mkutano huo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 18, 2016 02:10 UTC
  • Balozi Mzayuni asababisha kufutwa mkutano Afrika Kusini

Mkutano uliokuwa ufanyike mjini Johannesburg, kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro wa maji nchini Afrika Kusini umefutwa kutokana na kulalamikiwa vikali kualikwa balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye mkutano huo.

Shirika la habari la Qudsuna limerioti habari hiyo na kusema kuwa, mkutano huo ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu wa Februari lakini umefutwa na hautafanyika tena baada ya kuzuka malalamiko mengi kutoka kwa harakati ya kimataifa ya kuisusia Israel kutokana na kualikwa balozi wa Israel nchini Afrika Kusini, Arthuth Lenk, kwenye mkutano huo.

Hii ni katika hali ambayo, Lorenzo Fioramonti, profesa wa masuala ya kiuchumi na kisiasa katika Chuo Kikuu cha Pretoria ambaye alipangiwa kuzungumza kwenye mkutano huo alishatangaza kususia mkutano huo kutokana na kualikwa balozi huyo wa Israel.

Alisema, kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha kuwa, vyanzo vya maji ya Wapalestina vimepotea kutokana na siasa za kibaguzi na za kupenda kujitanua za Israel na kwamba si jambo linalokubalika kujaribu kuficha jinai hizo kupitia kuitisha mijadala kama hiyo na kuwapa nafasi ya kujitetea Wazayuni.