Radiamali ya Hamas kwa vitisho vya Waziri wa Vita wa Israel
(last modified Tue, 25 Oct 2016 08:19:21 GMT )
Oct 25, 2016 08:19 UTC
  • Radiamali ya Hamas kwa vitisho vya Waziri wa Vita wa Israel

Harakati ya Mapambano wa Kiislamu ya Palestina Hamas imepuuzilia mbali vitisho vilivyotolewa hivi karibuni na waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel, Avigdor Lieberman, akidai kuwa utawala huo utausambaratisha muqawama wa Wapalestina.

Hazem Kassem, msemaji wa Hamas amesema matamshi hayo ya Lieberman ni ya kipuuzi na hayana maana yeyote na kusisitiza kuwa, muaqawama wa Palestina hauwezi kuvunjwa na maneno matupu.

Jumatatu ya jana, waziri wa vita wa Israel aliliambia gazeti la Palestina la al-Quds kuwa, jeshi la utawala haramu wa Israel litaisabaratisha kikamilifu harakati ya Hamas katika siku za usoni huko Ukanda wa Gaza.

Waziri wa vita wa Israe, Avigdor Lieberman

Haya yanajiri siku chache baada ya kamanda wa zamani wa jeshi la Israel kukiri kuwa ni vigumu kuifuta Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas. Akizungumza kwenye mahojiano na gazeti la Kizayuni la Haaretz, Jenerali Gadi Shamni kamanda mstaafu wa jeshi la Israel amekiri kuwa, ni vigumu kuifuta harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas katika eneo la Ukanda wa Gaza.

Hii ni katika hali ambayo, taasisi karibu 80 za Palestina zimetahadharisha kuhusu hali mbaya ya kibinadamu huko katika Ukanda wa Gaza na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa kuwajibika ili kuondoa mzingiro wa kidhulma uliowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hilo na pia kuharakisha mchakato wa kuijenga upya Gaza. 

Vilevile kukatwa kwa muda mrefu umeme unaoingia Ukanda wa Gaza kumezidisha matatizo ya raia milioni moja na laki tisa wa eneo hilo lililo chini ya mzingiro wa pande zote wa Israel.

Tags