Israel yawafungia watoto zaidi wa Palestina huko Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i1867-israel_yawafungia_watoto_zaidi_wa_palestina_huko_quds
Waziri wa Palestina anayeshughulikia hali ya wafungwa walioko kwenye jela za utawala haramu wa Israel amesema leo kuwa watoto wasiopungua 60 wa Kipalestina wamewekwa chini ya vifungo vya nyumbani katika mji wa Quds.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 24, 2016 11:03 UTC
  • Israel yawafungia watoto zaidi  wa Palestina huko Quds

Waziri wa Palestina anayeshughulikia hali ya wafungwa walioko kwenye jela za utawala haramu wa Israel amesema leo kuwa watoto wasiopungua 60 wa Kipalestina wamewekwa chini ya vifungo vya nyumbani katika mji wa Quds.

Issa Qaraqe amesema utawala haramu wa Israel unawazuia watoto hao kupata masomo na matibabu kama watoto wengine; jambo linalokiuka haki zao za ki msingi. Waziri Qaraqe ametoa mfano wa Musa Najib, kijana mwenye umri wa miaka 16 ambaye amewekwa chini ya kifungo cha nyumbani hadi mwezi Julai wakati wa kusikizwa kwa kesi yake na kusema huo ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Mama ya Najib ametakiwa kuhakikisha mtoto wake hakiuki masharti ya kifungo chake la sivyo asukumwe jela pamoja na mwanawe. Qaraqe anasema kuna watoto walio chini ya umri wa miaka 12 ambao nao pia wamewekwa chini ya vifungo vya nyumbani na utawala bandia wa Israel. Huku hayo yakijiri, ripoti mpya zinasema kuwa, wanajeshi wa Israel wamekuwa wakiwatesa Wapalestina wakati wa kuwasaili. Mashirika mawili ya haki za binadamu ya huko Israel yamesema mbinu za mateso zinazotumiwa na vyombo vya usalama vya utawala ghasibu zinahesabiwa kuwa jinai dhidi ya binadamu.