Saudia inaendelea kutoa misaada ya kifedha kwa magaidi Syria
Saudia Arabia hivi karibuni imetoa msaada mwingine wa Riali Milioni 100 za Kisaudi ($ Milioni 26.5) kwa ajili ya magaidi nchini Syria.
Kwa mujibu wa tovuti ya Ajel ya Syria, Mfalme Salman bin Abdul Aziz wa Saudia ametoa amri ya kuzinduliwa mpango maalumu wa kampeni ya mchango wa pesa kwa kisngizio cha kuwasaidia watu wa Syria. Hata hivyo, tovuti hiyo imefichua kuwa tayari kitita cha Dola Milioni 26.5 ambacho kimedaiwa ni cha wakimbizi kimetumika kununua silaha zinazotumiwa na magaidi nchini Syria.
Tovuti hiyo imesema kuwa siku ya Jumatatu Mohammad bin Nayef, Mritihi wa Kitu cha Ufalme alitoa mchango wa Riali milioni 10 naye Mohammad bin Salman Waziri wa Ulinzi wa Saudia akatoa milioni 8 katika kampeni hiyo ya misaada ya magaidi iliyojifichwa nyuma ya pazia la misaada kwa wakimbizi.
Tokea mgogoro wa Syria uanze mwaka 2011 Saudia imekuwa muungaji mkono mkuu wa magaidi ambapo huwatumia magaidi silaha katika misafara inayodaiwa kuwa imesheheni misaada ya kibinadamu.
Hivi karibuni Jeshi la Syria lilifanikiwa kuukomboa mji wa Aleppo uliokuwa unakaliwa kwa mabavu na magaidi wanaopata himaya ya Saudi Arabia na Qatar.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Adel al Jubeir, kabla ya kukombolewa Aleppo, alisema nchi yake imewapa magaidi Syria mfumo wa makombora ya anga na zana nyinginezo za kivita.