Syria yaendeleza oparesheni dhidi ya magaidi karibu na Damascus
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i22258-syria_yaendeleza_oparesheni_dhidi_ya_magaidi_karibu_na_damascus
Jeshi la Syria limeanzisha oparesheni kali ya kuwapokonya magaidi udhibiti wa eneo la kistratijia karibu na Damascus ambalo lina chemichemi ambayo maji yake yanatumika katika mji mkuu huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 27, 2016 23:21 UTC
  • Syria yaendeleza oparesheni dhidi ya magaidi karibu na Damascus

Jeshi la Syria limeanzisha oparesheni kali ya kuwapokonya magaidi udhibiti wa eneo la kistratijia karibu na Damascus ambalo lina chemichemi ambayo maji yake yanatumika katika mji mkuu huo.

Ndege za kivita za  Syria zimetekeleza mashambulizi kadhaa katika ngome za  magaidi katika eneo la bonde linaitwa Wadi Barada yapata kilomita 18 kaskazini magharibi mwa mji mkuu.

Siku kadhaa zilizopita magaidi wakufurishaji wanaodhibiti eneo hilo walimwaga diseli kwenye maji ya chemichemi hiyo ili wakaazi wa Damascus wasiweze kuyatumia. Halmasharui ya Maji mjini Damascus ililazizmika kukata maji ya bonde hilo na kulazimika kutafuta vyanzo vingine vya maji baad aya magaidi kumwaga diseli katika chemichemi hiyo inayojulikana kama al Fija.

Magaidi wa ISIS au Daesh

Hayo yanajiri siku kadhaa baada ya jeshi la Syria kuukomboa mji wa Aleppo ambao ulikuwa unakaliwa na magaidi tokea mwaka 2012.

Serikali ya Syria imekuwa ikisisitiza kuwa magaidi nchini humo wanapata misaada ya kifedha na kisilaha kutoka kwa nchi za Magharibi hasa Marekani na waitifaki wake katika eneo hili ambao ni Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na utawala haramu wa Israel. Karibu watu nusu milioni wameshapoteza maisha tokea magaidi waanzishe kampeni ya kumuondoa madarakani Rais Bashar al Assad wa Syria mwaka 2011.