Israel yaingiwa na kiwewe kuhusu uwezo wa Hizbullah
Kituo kimoja cha utafiti katika utawala wa Kizayuni wa Israel kimekiri katika ripoti yake ya hivi karibuni kuwa, Wazayuni wana wasiwasi mkubwa kuhusu nguvu za harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
Kituo cha Utafiti wa Usalama wa Ndani cha Utawala wa Kizayuni wa Israel kimetoa ropoti kuhusu kiwango cha hatari zinazoukabli utawala huo katika mwaka mpya wa 2017 na kusema, 'Hizbullah ya Lebanon ni tishio kubwa zaidi kwa Israel'.
Kabla ya ripoti hiyo, Yair Golan, Naibu Mkuu wa Komandi ya Pamoja ya Jeshi la Utawala wa Kizayuni wa Israel alikiri kuwa Hizbullah imeimarisha uwezo wake, na kwamba harakati hiyo ya Kiislamu imebadilika na kuwa tishio lisilo na kifani kwa Israel.
Kituo cha Utafiti wa Usalama wa Ndani cha Israel kimewataka wakuu wa utawala huo kupata funzo kutoka vita vya huko nyuma na kujitayarisha kijeshi kwa mapigano yoyote yanayoweza kutokea.
Katika vita vya siku 33 vya utawala wa Kizayuni wa Israel na Lebanon mwaka 2006, utawala huo ulishindwa vibaya na kupata hasara kubwa ya kifedha huku idadi kubwa ya askari wake wakiuawa katika mapigano na Hizbullah. Hatimaye utawala huo ulilazimika kurudi nyuma na ndipo vita vikamalizika.