HAMAS: Mkutano wa Paris kuhusu Palestina ni kupoteza wakati
(last modified Mon, 16 Jan 2017 03:51:43 GMT )
Jan 16, 2017 03:51 UTC
  • HAMAS: Mkutano wa Paris  kuhusu Palestina ni kupoteza wakati

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, mkutano wa mapatano ulioanza jana huko Paris Ufaransa ni kupoteza wakati bure na ni marudio ya mikutano ya mapatano ya huko nyuma ambayo haikuwa na matunda yoyote.

Sami Abu Zuhri msemaji rasmi wa Harakati ya Muqawama ya Palestina HAMAS sambamba na kuwakosoa vikali waandaaji wa mkutano huo wa Paris kuhusu Palestina amebainisha kwamba, mkutano huo unafanyika huku kukiongezeka mashambulio na hujuma za Isrrael dhidi ya Wapalestina na kuendelea ujenzi wa vitongoji vya waowezi wa Kiyahudi na hapana shaka kuwa, mkutano huo hautakuwa na msaada wowote ule kwa kadhia ya Palestina.

Msemaji huyo wa Hamas amesisitiza kuwa, kufanyika mkutano huo katika mazingira kama haya wanayokabiliwa nayo Wapalestina ni kupoteza wakati.

Bendera ya Palestina

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeitaka serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina kutokuwa na matumaini na hatua kama hiyo isiyo na faida na badala yake ifanye hima ya kupatikana amani na kuhitimishwa hitilafu za ndani baina ya Wapalestina.

Wakati huo huo, Mustafa Barghouthi Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubunifu wa Kitaifa wa Palestina naye amekosoa vikali mkutano huo wa Paris na kubainisha kwamba, tatizo lubwa la mkutano huo ni kwamba, hautaki Israel iwekewe vikwazo na kuadhibiwa.

Mkutano wa kimataifa kuhusu Palestina ulianza jana Jumapili katika mji mkuu wa Ufaransa Paris ukihudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi 70 duniani na lengo lake ni kuhuisha mwenendo wa mapatano baina ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina na utawala haramu wa Israel.

Tags