Russia yakanusha kuuliwa wanajeshi wake Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i24745-russia_yakanusha_kuuliwa_wanajeshi_wake_syria
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia amekanusha ripoti iliyotolewa kuhusu kuuliwa wanajeshi wake huko Syria.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Feb 05, 2017 23:12 UTC
  • Russia yakanusha kuuliwa wanajeshi wake Syria

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia amekanusha ripoti iliyotolewa kuhusu kuuliwa wanajeshi wake huko Syria.

Igor Konashenkov Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia ameeleza kuwa ripoti iliyotolewa na kanali ya televisheni ya al Jazeera kuhusu kuuawa wanajeshi watano wa Russia kufuatia kulipuka gari la kijeshi la nchi hiyo katika mji wa Ladhiqiya huko Syria ni ya uwongo. Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia ameeleza kuwa wanajeshi wake wote walioko Syria wako salama salimini na wanatekeleza majukumu yao kama kawaida. Kanali ya televisheni ya al Jazeera Jumamosi iliyopita ilitangaza kuwa, wanajeshi watano wa Russia wameuawa baada ya gari moja la jeshi la Syria waliokuwa wamepanda kulipuka katika mji wa Ladhiqiya. 

Baadhi ya wanajeshi wa Russia walioko Syria