Kusimama kidete wananchi wa Yemen, sababu ya uadui wa Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i24973-kusimama_kidete_wananchi_wa_yemen_sababu_ya_uadui_wa_saudia
Katibu Mkuu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, utawala wa Saudi Arabia unamshambulia mtu yoyote ambaye anaipinga Israel na kukabiliana na siasa za Marekani.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Feb 10, 2017 21:51 UTC
  • Kusimama kidete wananchi wa Yemen, sababu ya uadui wa Saudia

Katibu Mkuu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, utawala wa Saudi Arabia unamshambulia mtu yoyote ambaye anaipinga Israel na kukabiliana na siasa za Marekani.

Sayyid Abdulmalik Badruddin alisema jana Ijumaa katika maadhimisho ya Siku ya Shahidi kuwa, lengo la uvamizi na mashambulizi ya Saudi Arabia dhidi ya Yemen ni kutokomeza uhuru na kupora utajiri wa nchi hiyo na kuongeza kuwa, nchi vamizi zimeshambulia na kuharibu kila kitu nchini Yemen ikiwa ni pamoja na kuwauwa raia, kuharibu miundombinu na kubomoa turathi za kale na za kihistoria za nchi hiyo. Katibu Mkuu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, miili iliyokatwa vipande vipande ya maelfu ya watoto wa Yemen, inathibitisha madai ya uongo ya nchi zilizoivamia Yemen na jinai za kutisha walizowatendea raia wa nchi hiyo. 

Jinai za Saudi Arabia dhidi ya wananchi wa Yemen 

Sayyid Abdulmalik Badruddin amesema Marekani na Israel kamwe hazitetei wala kuheshimu haki yoyote duniani na kueleza kuwa, tawala za kieneo ndizo zilizopanga njama za kuivamia Yemen. Ameongeza kuwa, uungaji mkono usio wa kimantiki wa Marekani, Israel na waitifaki wao kwa nchi vamizi dhidi ya Yemen unasikitisha na kusisitiza kuwa, Wayemen watatumia uwezo wao wote kupambana na chokochoko hizo za nchi ajinabi ili kuilinda nchi yao.