Hamas yasisitiza umuhimu wa mkutano wa kuiunga mkono Intafadha ya Palestina
(last modified Sun, 19 Feb 2017 14:58:51 GMT )
Feb 19, 2017 14:58 UTC
  • Hamas yasisitiza umuhimu wa mkutano wa kuiunga mkono Intafadha ya Palestina

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesisitiza umuhimu mkubwa wa Mkutano wa Sita wa Kuiunga Mkono Intifadha na Quds katika mazingira ya sasa katika eneo na duniani kwa ujumla utakaofanyika hapa Tehran.

Tahir al Nunu mmoja wa viongozi wa harakati ya Hamas ya Palestina amesisitiza kuwa Mkutano wa Kuiunga Mkono Intifadha na Quds utakaofanyika Tehran ni dhahir shahir kuwa unatilia mkazo kuhusu chaguo la muqawama kama njia pekee ya kistratejia katika eneo. Kabla ya hapo pia viongozi wa Hamas akiwemo Mahmoud al Zahar walisisitiza kuhusu umuhimu wa mkutano huu wa Tehran na kusema kuwa wanafanya juhudi ili watume ujumbe wa ngazi ya juu wa harakati hiyo kushiriki mkutano huo. 

Mahmoud al Zahar mmoja wa viongozi wa Harakati ya Hamas ya Palestina 

Hazem Qassim msemaji wa harakati ya Hamas siku kadhaa zilizopita alisema kuwa ujumbe wa ngazi ya juu wa harakati hiyo utashiriki katika mkutano wa Tehran wa Kuiunga Mkono Intifadha ya Palestina na Quds. Mkutano wa Sita wa Kuiunga Mkono Intifadha na Quds utaanza kesho kutwa hapa Tehran kwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa nchi za Kiislamu. 

Tags