Wapalestina waushitaki utawala haramu wa Israel katika mahakama ya ICC
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i26522-wapalestina_waushitaki_utawala_haramu_wa_israel_katika_mahakama_ya_icc
Mwenyekiti wa Kituo cha Haki za Binadamu cha Palestina Radhi al Surani amesema kuwa kutuo hicho kimewasilisha mashtaka sita dhidi ya utawala haramu wa Isarel katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 17, 2017 23:18 UTC
  • Wapalestina waushitaki utawala haramu wa Israel katika mahakama ya ICC

Mwenyekiti wa Kituo cha Haki za Binadamu cha Palestina Radhi al Surani amesema kuwa kutuo hicho kimewasilisha mashtaka sita dhidi ya utawala haramu wa Isarel katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).

Al Surani amesema mashtaka hayo yanahusiana na uhalfu uliofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza, kulizingira eneo hilo na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi ya Palestina licha ya Umoja wa Mataifa kupiga marufuku suala hilo. 

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ndiyo mahakama pekee ya kimataifa inayoweza kushughulikia watu binafsi na viongozi kwa tuhuma za kutenda jinai bila ya kujali kinga zao za kisheria. Palestina ilipata uanachama katika mahakama hiyo mwaka 2015 na kwa msingi huo imefungua mashtaka dhidi ya viongozi wa utawala ghasibu wa Isarel kwa kutenda jinai za aina mbalimbali dhidi ya watu wa Palestina. 

Hapa linakuja swali kwamba ni mashtaka yepi yanayoweza kuwasilishwa na Palestina katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai dhidi ya Israel? Kwa mujibu wa hati ya Roma iliyounda mahakama ya ICC, mahakama hiyo inaweza kushughulikia kesi za mauaji ya kimbari (genocide), jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu na uhalifu wa ubakaji.  

Watoto ndio wahanga wakubwa wa mashambulizi ya Israel, Palestina

Utawala ghasibu wa Israel umetenda jinai zote hizo zilizotajwa katika hati ya mahakaya ya ICC huko Palestina. Mzingiro wa Gaza ambao sasa unaingia mwaka wa 11 ni kielelezo cha mauaji ya kimbari. Mzingiro huo wa pande zote za nchi kavu, angani na baharini umesababisha mgogoro mkubwa wa kibinadamu unaoandamana na na ukosefu wa bidhaa muhimu kama chakula, dawa, maji na kadhalika na kusababisha maradhi na vifo vya watu hususan watoto, wanawake na watu wazima. Israel iliweka mzingiro huo wa kuzuia bidhaa zote kuingia na kutoka Ukanda wa Gaza kwa shabaha ya kuangamiza kizazi chote au baadhi ya wakazi wa Gaza.

Kwa mujibu wa kifungu cha 6 cha hati ya Maharaka ya Kimataifa ya Jinai, uhalifu kama ule wa kusababisha madhara makubwa kwa mwili au madhara ya kinafsi na kuwalazimisha watu wa jamii au kundi kukimbia kunakopelekea kuangamia kwao, vinatambuliwa kuwa ni kielelezo cha mauaji ya kimbari.

Vita vya Israel dhidi ya watu wa Palestina hapo mwaka 2014 na kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina pia ni vielelezo vya jinai dhidi ya binadamu. Vita hivyo vilipelekea kuuawa shahidi Wapalestina zaidi ya 2200 na maelfu ya wengine kujeruhiwa. Jinai za Israel huko Palestina pia zimewalazimisha mamilioni ya Wapalestina kuwa wakimbizi katika maeneo mbalimbali duniani. Wakati huo huo ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi za Ukingo wa Magharibi umewalazimisha wakazi wa maeneo hayo kuwa wakimbizi na kuwa kielelezo cha kuangamiza kizazi cha watu.

Watu wa Gaza wanaishi katika hali mbaya na dhidi kubwa

Mahakama ya Kimataifa y Jinai (ICC) inaweza kushughulikia kesi za uhalifu uliofanyika baada ya mwaka 2002 yaani baada ya kuanza kutekelezwa hati ya mahakama hiyo. Kwa msingi huo serikali ya Palestina pia inaweza kuwasilisha mashtaka ya jinai zilizofanywa na israel katika mahakama hiyo ikizingatiwa wakati zilipotendwa na Wazayuni maghasibu.

Kwa kutilia maanani kwamba, katika shughuli za Mahakama ya Kimataifa ya Jinai hakuna nchi au jaji mwenye mamlaka makubwa zaidi kuliko nchi au jaji mwenzake, wala hakuna haki ya veto katika maamuzi ya mahakama hiyo, inatazamiwa kuwa, mashtaka yaliyowasilishwa na Palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel yatakuwa na matunda ya kuridhisha kwa watu wa Palestina.