Wapalestina waandamana kulaani ukatili wa Israel
Mamia ya Wapalestina wameshiriki katika mazishi ya kiijana aliyeuawa kwa kupigwa risasia na vikosi vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji wa Al Khalil huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Mazishi hayo ya Jumamosi yaligeuka na kuwa maandamano ya kulaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wasio na hatia wa Palestina.
Mazishi na maandamano hayo yalifanyika Jumamosi katika kambi ya wakimbizi ya Arroub ambapo Wapalestina walikuwa wanaomboleza kuuawa shahidi kijana Murad Yusuf Abu Ghazi. Kijana huyo aliyekuwa na umri wa miaka 16 alipoteza maisha mapema Jumamosi baada ya wanajeshi wa Israel kumfyatulia risasi na kumuua kwa madai kuwa eti alikuwa anapanga kuwashambulia.
Mazishi ya Shahidi Yusuf yalifanyika masaa machache baada ya mazishi mengine huko Beit Lahm ya mwanaharakati wa Palestina Basil al Araj ambaye aliuawa shahidi na wanajeshi katili wa Israel mjini Ramallah wiki mbili zilizpoita.
Mpalaestina huyo aliyekuwa na umri wa miaka 31 alimiminiw risasi na baada ya hapo mwili wake kutekwa na Wazayuni kabla ya kukabidhiwa familia yake Ijumaa alasiri.
Araj alikuwa anaheshimika kama mpigania ukombozi wa Palestina, msomi na mwananadharia. Kuuawa kwake shahidi mikononi mwa askari wa Kizayuni ni jambo ambalo liliibua hasira miongoni mwa Wapalestina.