Israel iliteka nyara Wapalestina 500 mwezi Machi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i27614-israel_iliteka_nyara_wapalestina_500_mwezi_machi
Utawala wa Kizayuni wa Israel uliwateka nyara Wapalestina 509 katika Ukanda wa Ghaza, Ukingo wa Magharibi na Quds Tukufu mwezi uliopita wa Machi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 11, 2017 02:01 UTC
  • Israel iliteka nyara Wapalestina 500 mwezi Machi

Utawala wa Kizayuni wa Israel uliwateka nyara Wapalestina 509 katika Ukanda wa Ghaza, Ukingo wa Magharibi na Quds Tukufu mwezi uliopita wa Machi.

Kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Jumuiya ya Mateka wa Wapalestina na Kituo cha Haki za Binadamu cha Al Mezan, waliokamatwa ni pamoja na watoto 75, wanawake 13 na waandishi habari watano. Aghlabu ya waliokamatwa walikuwa katika mji wa Quds.

Idadi ya mateka wa Kipalestina walioko katika jela za Israel wamefikia elfu saba kutokana na siasa zinazotekelezwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestina; huku takwimu zikionyesha kuwa wafungwa wengi wamepata maradhi yasiyotibika.

Wapalestina katika moja ya jela za kuogofya za Israel

Utawala wa Kizayuni unashadidisha jinai zake dhidi ya raia wa Palestina na kukaidi kutekeleza maazimio ya kimataifa likiwemo azimo la Geneva linalohusu mateka wa Kipalestina.

Aidha idadi kubwa ya mateka wa Kipalestina wanafungwa na kuteseka katika jela za utawala pandikizi wa Israel bila ya kuelezwa makosa yao au kufunguliwa mashtaka.