Wazayuni waendelea kuwanyanyasa Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i27924-wazayuni_waendelea_kuwanyanyasa_wapalestina
Wimbi la unyanyasaji dhidi ya viongozi wa mateka wa Kipalestina katika jela za kutisha za Israel limeendelea kwa wanajeshi wa utawala huo dhalimu kuwahamishia mateka wa Palestina wanaogoma kula katika jela ya kuogofya ya Jalama ya Kizayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 18, 2017 03:40 UTC
  • Wazayuni waendelea kuwanyanyasa Wapalestina

Wimbi la unyanyasaji dhidi ya viongozi wa mateka wa Kipalestina katika jela za kutisha za Israel limeendelea kwa wanajeshi wa utawala huo dhalimu kuwahamishia mateka wa Palestina wanaogoma kula katika jela ya kuogofya ya Jalama ya Kizayuni.

Kituo cha upashaji habari ya Palestina kimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, wakuu wa jela za utawala wa Kizayuni, jana waliwahamishia kwenye jela hiyo viongozi sita wa mateka wa Palestina waliogoma kula kutokana na unyanyasaji mkubwa wanaofanyiwa na Wazayuni.

Wakati huo huo Yisrael Katz, waziri wa habari, uchukuzi na mawasiliano wa utawala wa Kizayuni ametaka kunyongwa mateka wote wa Kipalestina wanaogoma kula.

Watoto wadogo wa Palestina ni wahanga wakuu katika jela za kuogofya za Israel

 

Amesema, kuna udharura wa kuwasilishwa tena muswada wa sheria ya kuwanyonga Wapalestina wote wanaogoma kula katika bunge la Israel.

Wakati huo huo Qadura Fares, mkuu wa taasisi ya mateka wa Kipalestina ameliambia shirika la habari la IRNA kwamba utawala wa Kizayuni na taasisi zake mbalimbali hususan zile zinazoendelesha jela na taasisi za usalama wa ndani ndizo zinazopaswa kubeba majukumu ya madhara yoyote wanayopata mateka wa Kipalestina wanaogoma kula.

Amesema, hatua ya mateka wa Palestina ya kuanzisha mgomo wa kula iliyoanza jana tarehe 17 Aprili, ambayo ilikuwa ni Siku ya Mateka wa Palestina, inashirikisha zaidi ya mateka elfu moja na 500 wa Kipalestina, na mgomo huo uko katika jela zote za utawala wa Kizayuni.