Rais Ghani wa Afghanistan amesema kiongozi wa ISIS nchini humo ameuawa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i28808-rais_ghani_wa_afghanistan_amesema_kiongozi_wa_isis_nchini_humo_ameuawa
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani amesema kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) nchini humo ameuawa katika mashambulizi ya pamoja ya jeshi la nchi hiyo na Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 08, 2017 03:21 UTC
  • Rais Ghani wa Afghanistan amesema kiongozi wa ISIS nchini humo ameuawa

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani amesema kiongozi wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh (ISIS) nchini humo ameuawa katika mashambulizi ya pamoja ya jeshi la nchi hiyo na Marekani.

Ghani amesema kamanda huyo mkuu wa Daesh kwa jina Abdul-Hasib ameuawa katika operesheni ya pamoja ya jeshi la Afghanistan na Marekani katika mkoa wa Nangarhar, mashariki mwa nchi.

Amesema kikosi hicho kilichomuangamiza kamanda huyo wa ISIS kilijumuisha makomandoo 50 wa Kiafghani na wanajeshi 50 wa Kikosi Maalumu cha Marekani.

Rais Ghani ameongeza kuwa, sehemu alikokuwa amejificha kiongozi huyo wa Daesh ni ngome ya kundi hilo la kigaidi iliyoshambuliwa kwa bomu linalofahamika kama 'Mama wa Mabomu Yote" la Marekani Aprili 13. 

Magaidi wa Daesh nchini Afghanistan

Bomu hilo la GBU-43B lina uzito wa tani 11 za mada za milipuko ya TNT na ndilo lenye uharibifu mkubwa zaidi kuliko mabomu yote yasiyo ya nyuklia duniani.

Rais wa Marekani Donald Trump alipongeza operesheni hiyo dhidi ya Afghanistan katika mkoa wa Kunar na kudai kuwa wanachama kati ya 700 na 1,500 wa kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS (Daesh) waliuawa.