Unicef: Kuna uhaba wa suhula za matibabu nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i31090-unicef_kuna_uhaba_wa_suhula_za_matibabu_nchini_yemen
Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umetahadharisha kuhusu taathira mbaya za hatua ya Saudi Arabia ya kuizingira Yemen na uhaba wa suhula za matibabu na dawa unaoikabili nchi hiyo maskini ya Kiarabu.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 29, 2017 04:11 UTC
  • Unicef: Kuna uhaba wa suhula za matibabu nchini Yemen

Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umetahadharisha kuhusu taathira mbaya za hatua ya Saudi Arabia ya kuizingira Yemen na uhaba wa suhula za matibabu na dawa unaoikabili nchi hiyo maskini ya Kiarabu.

Vile vile shirika la Unicef limetahadharisha kuwa hatua ya Saudia ya kuizingira Yemen imelifanya gumu zoezi la kutuma vifaa vya tiba na madawa huko Yemen.

Taarifa ya shirika hilo la kimataifa imeongeza kuwa, makumi ya tani za misaada ya tiba tayari imetumwa Yemen ili kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu huku Shirika la Afya Duniani (WHO) pia likitangaza kuwa watu laki mbili wanaugua kipindupindu nchni Yemen. 

Maafa yaliyosababishwa na mashambulizi ya Saudia nchini Yemen 

Utawala wa Aal Saud ulianzisha mashambulizi ya kijeshi nchini Yemen mwezi Machi mwaka juzi lengo likiwa ni kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake rais wa zamani wa nchi hiyo Abdu Rabbu Mansour Hadi.

Hadi hivi sasa mashambulizi hayo yameshauwa na kujeruhi maelfu ya raia wa Yemen na kusababisha maafa makubwa kwa miundombinu duni ya kiuchumi ya nch hiyo. Taasisi mbalimbali za kimataifa wameitaja hatua ya Saudia na nchi waitifaki wake ya kuanzisha vita vya kivamizi huko Yemen kuwa ni jinai ya kivita.