Misri na Marekani zaendeleza tuhuma zao dhidi ya Qatar
(last modified Tue, 04 Jul 2017 07:55:41 GMT )
Jul 04, 2017 07:55 UTC
  • Misri na Marekani zaendeleza tuhuma zao dhidi ya Qatar

Kwa mara nyingine Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na Misri wameituhumu Qatar kwamba, inaunga mkono ugaidi, kuingilia masuala ya ndani ya nchi majirani na kufanya mahusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Sameh Shoukry Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amefanya amezungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Rex W. Tillerson juu ya mgogoro unaoendelea baina ya Saudia na Qatar. Katika mawasiliano hayo, Rex W. Tillerson na Sameh Shoukry mbali na kujadili mgogoro huo, wamezungumzia pia matukio ya eneo la Mashariki ya Kati  na namna ya kuinua mahusiano ya nchi mbili.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Misri na Marekani

Wakizungumzia suala la Qatar, mawaziri hao wa Misri na Marekani wameikosoa serikali ya Doha kwa kile walichodai kuwa, eti inaunga mkono ugaidi, kuingilia masuala ya ndani ya nchi za jirani na kadhalika kuwa karibu na Iran. Hii ni katika hali ambayo awali serikali ya Washington ilitangaza azma yake ya kutokuwa upande wowote katika mgogoro. Itakumbukwa kuwa tarehe tano Juni nchi za Misri, Imarati na Bahrain zikiongozwa na Saudia zilitangaza kukata mahusiano yao ya kidiplomasia na Qatar, sambamba na kuiwekea mzingiro wa angani, nchi kavu na baharini. Katika fremu hiyo hiyo tarehe 23 ya mwezi Juni, mataifa hayo ya Kiarabu yaliiwekea serikali ya Doha masharti 13 na kudai kuwa, yatakuwa tayari kufungua ukurasa mpya na Qatar, ikiwa ingeyatekeleza, masharti ambayo hata hivyo yametupiliwa mbali na nchi hiyo.

Mgogoro wa Saudia na Qatar

Moja ya masharti hayo ilikuwa ni kuitaka Qatar kukata mahusiano yake ya kila upande na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Harakati ya Kiislamu ya Hizbullah, Harakati ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na kadhalika kufunga kikamilifu ofisi za kanali za al-Jazeera.

Tags