Qatar kuishtaki Imarat kwa kuhusika na udukuzi
(last modified Tue, 18 Jul 2017 15:14:46 GMT )
Jul 18, 2017 15:14 UTC
  • Qatar kuishtaki Imarat kwa kuhusika na udukuzi

Serikali ya Qatar imeeleza kusikitishwa sana na hatua ya Imarat ya kudukua mitandao ya intaneti ya serikali ya Doha, suala ambalo limeibuka mgogoro wa sasa kati ya nchi hizo mbili na kusisitiza kuwa, Doha itawafungulia mashtaka wahusika wa uhalifu huo.

Saif bin Ahmad Al Thani, mkuu wa Idaraya Mawasiliano ya serikali ya Qatar sambamba na kuashiria habari iliyoandikwa na gazeti Washington Post la Marekani ambalo limefichua kuwa Imarat ndio iliyohusika na udukuaji wa mitandao ya intaneti ya serikali ya Doha, amesema kuwa hatua hiyo ni ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa, makubaliano ya Baraza la Ushirikiano la Ghuba la Uajemi, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League), Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Umoja wa Mataifa.

Ripoti ya gazeti la Washington Post

Amesema kuwa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Qatar anaendelea na uchunguzi kuhusiana na suala hilo na kwamba baada ya kumaliza shughuli hiyo atawachukulia hatua kali wahusika wote wa udukuaji huo.

Hivi karibuni maafisa wa mashirika ya ujasusi ya Marekani walitangaza kuwa, uchunguzi wao wa kiintelijensia umegundua kuwa, Umoja wa Falme za Kiarabu yaani Imarati ndio uliodukua mitandao ya intaneti ya serikali ya Qatar na kuingiza maneno ya uongo ili yaonekane yamesemwa na Amir wa nchi hiyo, Tamim bin Hamad Aal Thani.

Mgogoro wa mataifa hayo

Viongozi wa Imarat akiwemo Anwar Mohammed Qarqash, Waziri Mshauri wa Masuala ya Kigeni wa nchi hiyo na kadhalika Yousef Al Otaiba, balozi wa Imarat nchini Marekani wamekanusha madai hayo ya Doha. Al-Otaiba, amedai kuwa, taarifa iliyochapishwa na gazeti la Washington Post kwamba nchi yake ndiyo iliyohusika na udukuaji huo ni ya uongo. 

Tags