Ubalozi mdogo wa Israel wafungwa New York, Netanyahu atishiwa kuuawa
(last modified Sat, 16 Sep 2017 08:17:34 GMT )
Sep 16, 2017 08:17 UTC
  • Ubalozi mdogo wa Israel wafungwa New York, Netanyahu atishiwa kuuawa

Ubalozi mdogo wa utawala haramu wa Israel mjini New York, Marekani umefungwa baada ya kupokea vitisho.

Televisheni ya utawala haramu wa Israel imetangaza kuwa, ubalozi wa Israel mjini New York umepokea kifurushi chenye mada nyeupe  na ndani kuna vitisho dhidi ya Waziri Mkuu wa utawala huo, Benjamin Netanyahu.

Baada ya kupokea kifurushi hicho cha vitisho masaa kadhaa tu baada ya Netanyahu kuwasili New York, ubalozi mdogo wa Israel mjini huko umefungwa na wafanyakazi wake wote wametakuwa kubakia ndani yake.

Askari wa usalama wa Marekani wamepelekwa haraka katika eneo la ubalozi huo.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliwasili New York jana usiku kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa Baraza Kuu la Um oja wa Mataifa. 

Tags