Hamas: Ukombozi wa Palestina unahijatia umoja wa kitaifa
(last modified Sat, 30 Sep 2017 16:27:44 GMT )
Sep 30, 2017 16:27 UTC
  • Hamas: Ukombozi wa Palestina unahijatia umoja wa kitaifa

Naibu Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, ukombozi wa Palestina na Quds tukufu na kukomeshwa uvamizi wa utawala haramu wa Israel kunahitaji umoja na mshikamano wa kitaifa.

Khalil Hayya amesema kuwa, Hamas itafanya kila liwezekanalo kwa ajili ya kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa wa Wapalestina. Ameongeza kuwa, vita vya Hamas dhidi ya adui Mzayuni vingali vinaendelea na havitasimama hadi pale ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zitakapokombolewa. 

Naibu Mkuu wa Idara ya Siasa ya Hamas amesema kuwa, mapambano ya ukombozi wa Palestina yanahitajia kuwepo mshikamano wa kitaifa kwa mujibu wa mipango ya kisiasa ili kuweza kulinda haki za wakimbizi wa Palestina, haki ya kurejea katika ardhi zao na kukombolewa ardhi yote inayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni wa Israel. 

Watoto wa Kipalestina wamekuwa wakimbizi, Gaza

Ripoti ya Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) inasema kuwa, uharibifu mkubwa wa nyumba za Wapalestina uliofanywa na Israel mwaka uliopita wa 2016 umewalazimisha maelfu ya raia wa Palestina kuwa wakimbizi.   

Tags