Ndege za Saudia zaendelea kubomoa misikiti nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i36831-ndege_za_saudia_zaendelea_kubomoa_misikiti_nchini_yemen
Ndege za kijeshi za Saudi Arabia zikishirikiana na za Marekani zimeendelea kubomoa misikiti, nyumba za raia na vituo vya serikali na vya watu binafsi katika maeneo mbalimbali ya Yemen.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Nov 26, 2017 10:05 UTC
  • Ndege za Saudia zaendelea kubomoa misikiti nchini Yemen

Ndege za kijeshi za Saudi Arabia zikishirikiana na za Marekani zimeendelea kubomoa misikiti, nyumba za raia na vituo vya serikali na vya watu binafsi katika maeneo mbalimbali ya Yemen.

Nyumba na misikiti kadhaa imebomolewa kabisa katika mji mkuu Sana'a kufuatia hujuma na mashambulio ya anga ya hivi karibuni kabisa ya ndege za kijeshi za Saudia, ambayo yamesababisha uharibifu mkubwa pia kwa vituo vya serikali. 

Miji mingine ambayo nayo imeshuhudia nyumba, misikiti na idara za serikali zikibomolewa ni ya maeneo ya kusini mwa nchi hiyo. 

Wakati huo huo hujuma na mashambulio ya jeshi vamizi la Saudia yamekabiliwa na majibu ya vikosi vya kujitolea vya wananchi vikishirikiana na jeshi la nchi hiyo. Wanajeshi kadhaa wa Saudia wameangamizwa katika mkoa wa Najran baada ya kambi yao kushambuliwa kwa makombora.

Uharibifu na bomoa bomoa inayofanywa na ndege za kijeshi za Saudia huko Yemen

Tangu mwezi Machi mwaka 2015, Saudia, ikisaidiwa na kuungwa mkono na baadhi ya nchi za Kiarabu na Marekani imeanzisha mashambulio ya kinyama dhidi ya Yemen kwa lengo la kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake Abd Rabbuh Mansur Hadi, rais wa nchi hiyo aliyejiuzulu na kuitoroka nchi.

Raia zaidi ya elfu 13  wa Yemen wameuawa, hasa wanawake na watoto, na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika uvamizi huo wa kijeshi huku Umoja wa Mataifa ukishindwa kuchukua hatua yoyote ya kuzuia jinai hizo za Saudia huko Yemen. Aidha watu zaidi ya laki sita wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kote Yemen huku wengine zaidi ya 2,000 wakifarikia dunia tokea mwezi Aprili mwaka huu