Hamas yaitaka PLO kuutekeleza kivitendo uamuzi wake
(last modified Wed, 17 Jan 2018 04:30:47 GMT )
Jan 17, 2018 04:30 UTC
  • Hamas yaitaka PLO kuutekeleza kivitendo uamuzi wake

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa, uamuzi wa Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO kuhusiana na tangazo la Rais Donald Trump wa Marekani kuhusu Beitul-Muqaddas utakkuwa na umuhimu pale PLO itakapoutekeleza kivitendo.

Fawzi Barhoum, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesisitiza kuwa, mtihani na majaribu ya kweli kuhusiana na uamuzi uliotangzwa na Baraza Kuu la Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO ni kuufanyia kazi uamuzi huo na kuandaa mikakati ya lazima kwa ajili ya hilo.

Msemaji huyo wa Hamas amesema kuwa, utangaulizi wa mikakati hiyo ni kuboresha hali ya Wapalestina kwa mujibu wa makubaliano ya Cairo Misri ya mwaka 2011 na kupambana na utawala ghasibu wa Israel.

Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani yay Palestina

Mkutano wa 28 wa Baraza Kuu la Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) uliofanyika Jumapili na Jumatatu wiki hii ulipinga vikali uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuitambua Baitul-Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel.

Akihutubia katika mkutano huo, Rais Mahmoud Abbas wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alisisitiza kwamba, taifa la Palestina katu halitakubaliana na mpango huo wa Trump kuhusu Baitul-Muqaddas.

Aidha Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina alitahadharisha kwamba, mamlaka hiyo itakata uhusiano wake na nchi yoyote ile ambayo itafuata uamuzi wa Marekani na kuuhamishia ubalozi wake huko Beitul-Muqaddas kutoka Tel-Aviv.

Tags