Jeshi la Israel lamuua shahidi kijana wa Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i40033-jeshi_la_israel_lamuua_shahidi_kijana_wa_palestina
Wanajeshi katili wa utawala haramu wa Israel wamemuua shahidi Mpalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kwa tuhuma kuwa alitaka kumdunga kisu askari wa Kizayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 07, 2018 04:41 UTC
  • Jeshi la Israel lamuua shahidi kijana wa Palestina

Wanajeshi katili wa utawala haramu wa Israel wamemuua shahidi Mpalestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, kwa tuhuma kuwa alitaka kumdunga kisu askari wa Kizayuni.

Mpalestina huyo ameuawa mapema leo katika mji wa al-Khalil (Hebron), kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Jeshi la Israel linadai kuwa, Mpalestina huyo aliuawa kwa kujaribu kumdunga kisu mlinzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni vya Karmei Tzur, na hapo mlinzi wa pili akimuua shahidi kwa kummiminia risasi.

Binti wa Kipalestina aliyeuawa hivi karibuni na askari katili wa Israel

Haya yanajiri katika hali ambayo, malalamiko yangali yanatolewa baada ya jeshi la Israel kumuua Ahmad Nassar Jarrar, Mpalestina anayetuhumiwa kumuua kiongozi wa kidini wa Kizayuni, Rabbi Raziel Shevach mwezi uliopita.

Hivi karibuni, Harakati ya Kimataifa ya Kuwatetea Watoto tawi la Palestina ilitangaza kuwa wanajeshi wa utawala wa Kizayuni mwaka uliopita wa 2017 uliwauwa shahidi watoto 15 wa Kipalestina katika eneo la Ukanda wa Ghaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds.