Wakristo Palestina walalamikia ukandamizaji wanaofanyiwa na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i40881-wakristo_palestina_walalamikia_ukandamizaji_wanaofanyiwa_na_israel
Askofu Mkuu wa Kanisa la Orthodox Mashariki huko Palestina amelalamikia vikali unyanyasaji na ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wakristo wa Palestina na kusema kuwa lengo la Israel ni kupunguza kabisa idadi ya Wakristo huko Palestina.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 26, 2018 03:59 UTC
  • Wakristo Palestina walalamikia ukandamizaji wanaofanyiwa na Israel

Askofu Mkuu wa Kanisa la Orthodox Mashariki huko Palestina amelalamikia vikali unyanyasaji na ukandamizaji unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wakristo wa Palestina na kusema kuwa lengo la Israel ni kupunguza kabisa idadi ya Wakristo huko Palestina.

Shirika la habari la IRIB limeripoti kuwa, Askofu Theophilos III jana Jumapili alisema kuwa, Israel inafanya mashambulizi ya kiuadui yaliyopangiliwa vizuri dhidi ya makanisa na hivi sasa imeongeza kasi katika mashambulizi hayo.

Amesema, Meya wa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu amepasisha sheria na kutoa amri za aibu kabisa za kudhibiti vyanzo vya fedha, mali na hesabu za benki za makanisa huko Palestina.

Utawala wa Kizayuni wa Israel hauheshimu watu wa dini yoyote huko Palestina

 

Askofu Mkuu wa Wakristo wa Palestina ameongeza kuwa, sheria na hatua hizo mpya zinazochukuliwa na Israel zinakanyaga maafikiano na mikataba yote ya kimataifa inayolinda haki za makanisa.

Malalamiko makali ya Askofu Mkuu wa Palestina kuhusu mashambulizi yaliyopangiliwa vyema ya utawala wa Kizayuni wa Israeli dhidi ya makanisa ya Palestina yametolewa katika hali ambayo, Yusuf al Mahmoud, msemaji wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina naye ameonya juu ya hatari ya siasa mpya za kodi zinazotekelezwa na Israel dhidi ya makanisa na misikiti katika mji wa Baytul Muqaddas (Yerusalemu).

Amesema, Israel haiheshimu makubaliano na mikataba yoyote ya kimatafaia kuhusu uhuru wa kuabudu.