Bin Salman aukingia kifua hadharani utawala haramu wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i42602-bin_salman_aukingia_kifua_hadharani_utawala_haramu_wa_israel
Katika hali ambayo jamii ya kimataifa inaendelea kulaani mauaji ya Wapalestina yaliyofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia amejitokeza hadharani na kuutambua utawala huo ghasibu, sambamba na kusisitiza kuwa Wazayuni wana haki juu ya ardhi yao.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 03, 2018 09:29 UTC
  • Bin Salman aukingia kifua hadharani utawala haramu wa Israel

Katika hali ambayo jamii ya kimataifa inaendelea kulaani mauaji ya Wapalestina yaliyofanywa na jeshi la utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia amejitokeza hadharani na kuutambua utawala huo ghasibu, sambamba na kusisitiza kuwa Wazayuni wana haki juu ya ardhi yao.

Katika mahojiano na gazeti la Marekani la Atlantic, Mohammad Bin Salman amesema kuwa, "Naamini kuwa kila mmoja popote pale alipo ana haki ya kuishi katika taifa lake lenye amani. Naamini kwamba Wapalestina na Waisraeli wana haki ya kuishi katika ardhi zao."

Amebainisha kuwa, utawala wa kifalme wa Aal-Saud hauna tatizo lolote na Mayahudi na kusisitiza kwamba Saudia na Israel zina mambo mengi yenye maslahi ya pamoja.

Bin Salman alipokutana na Rais Donald Trump huko Marekani hivi karibuni

Bin Salman ameongeza kuwa, baada ya kupatiwa ufumbuzi mgogoro kati ya Israel na Palestina, Riyadh itaimarisha uhusiano wa kibiashara wa pande mbili na Tel Aviv sambamba na kuwa na uhusiano wa kawaida.

Siku ya Ijumaa, Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudia ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa utawala huo wa kiukoo alikutana na kufanya mazungumzo na wakuu wa makundi kadhaa ya kulobi ya utawala haramu wa Israel katika safari yake nchini Marekani.