Radiamali ya Hamas kufuatia kuuliwa Fadi al Batsh nchini Malaysia
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeutuhumu utawala wa Kizayuni kuwa umehusika kumuua Fadi al Batsh mwanachama wa harakati hiyo na kutahadharisha kuwa italipiza kisasi damu ya raia huyo wa Palestina.
Fadi Muhammad al Batsh mwanasayansi mtajika wa Kipalestina aliyekuwa na umri wa miaka 35 ambaye aliwahi kupokea tuzo bora ya utafiti katika Ulimwengu wa Kiarabu aliuawa shahidi jana alfajiri na watu wasiojulikana wakati akitoja katika Sala ya alfajiri kwenye msikiti mئoja huko Kuala Lumpur mji mkuu wa Malaysia.
Shirika la habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limeripoti kuwa Ismail Hania Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Palestina (Hamas) amelitaja Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) kuwa limehusika na mauaji hayo ya Fadi Muhammad al Batsh mwanasayansi huyo wa Kipalestina na aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu huko Kuala Lumpur Malaysia.
Ismail Hania amebainisha kuwa al Batsh ameacha rekodi na utendaji unaong'ara katika elimu ya sayansi, imani na kuhudumia malengo na wananchi wa Palestina na vile vile umma wa Kiislamu na wanadamu wote.
Katika upande mwingine, Naftali Bennett Waziri wa Elimu wa utawala wa Kizayuni amesema katika mahojiano na kanali ya saba ya televishenii ya utawala huo kuwa hakutatolewa ruhusa ya kuusafirisha mwili wa Fadi al Batsh hadi pale wanajeshi wa Israel waliotiwa mbaroni na Hamas watakaporejeshwa. Msomi huyo mtajika wa Palestina ambaye pia alikuwa mhandishi wa masuala ya umeme ameuliwa shahidi huko Malaysia ظikiwa zimepita siku kadhaa baada ya Yisrael Katz Waziri wa Habari wa utawala wa Kizayuni kutishia kuwaua viongozi na wanachama wa makundi ya Kipalestina khususan wa harakati za Jihadul Islami na Hamas.