Saeb Erekat: Hatutoshiriki katika mpango wa mapatano utakaopendekezwa na Trump
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i43828-saeb_erekat_hatutoshiriki_katika_mpango_wa_mapatano_utakaopendekezwa_na_trump
Katibu wa kamati ya utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) ametangaza kuwa, Wapalestina hawatashiriki katika mpango wowote ule wa mapatano utakaopendekezwa na rais wa Marekani, Donald Trump.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 29, 2018 22:10 UTC
  • Saeb Erekat: Hatutoshiriki katika mpango wa mapatano utakaopendekezwa na Trump

Katibu wa kamati ya utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) ametangaza kuwa, Wapalestina hawatashiriki katika mpango wowote ule wa mapatano utakaopendekezwa na rais wa Marekani, Donald Trump.

Saeb Erekat amebainisha kwamba, hatua ya Trump ya kuitambua Beitul-Muqaddas kuwa eti mji mkuu wa utawala haramu wa Israel na kufanya njama za kuondolewa katika meza ya mazungumzo suala la wakimbizi wa Kipalestina kurejea makwao kumeifanya Marekani itoke katika mkondo wa mchakato wa mazungumzo ya mapatano.

Katibu wa kamati ya utendaji ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina (PLO) amesisitiza kuwa, Marekani haiwezi kuwa mshirika au mpatanishi wa mwenendo wa mazungumzo ya mapatano isipokuwa kama itabadilisha msimamo wake kuitambua Beitul-Muqaddas kama mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel.

Rais Donald Trump wa Marekkani

Tarehe 6 Disemba mwaka jana Rais Donald Trump wa Marekani alichukua hatua ambayo ni kinyume na maazimio ya kimataifa ya kuitangaza Quds Tukufu kuwa eti mji mkuu wa utawala haramu wa Israel. Aidha rais huyo wa Marekani alitangaza kuwa serikali ya Washington imeanzisha mchakato wa kuuhamishia ubalozi wake katika mji huo kutoka Tel Aviv.

Uamuzi huo wa Trump ulilaaniwa na unaendelea kulaaniwa kila pembe ya dunia hususan katika ulimwengu wa Kiislamu.