Hamas yaonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i4507-hamas_yaonya_kuhusu_hali_mbaya_ya_kibinadamu_ghaza
Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina, Hamas, ameonya kuhusu maafa ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza kutokana na mzingiro wa kinyama wa utawala haramu wa Israel katika eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 06, 2016 02:59 UTC
  • Hamas yaonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu Ghaza

Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina, Hamas, ameonya kuhusu maafa ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza kutokana na mzingiro wa kinyama wa utawala haramu wa Israel katika eneo hilo.

Imad al Baz, naibu mkurugenzi wa Wizara ya Uchumi ya Gaza amesema uamuzi wa utawala haramu wa Israel kuzuia uingizaji wa saruji au simiti eneo hilo ni jambo litakalosimamisha ustawi wa kiuchumi, kuongeza ukosefu wa ajira na hivyo kuathiri vibaya maisha ya makumi ya maelfu ya Wapalestina.

Jumatatu, utawala wa Kizayuni wa Israel ulitangaza uamuzi wa kuzuia simiti kuingia Ghaza kama njia ya kuzidisha mzingiro katika eneo hilo. Hatua hiyo inamaanisha mamia ya miradi ya maendeleo Ghaza itasimaishwa. Miradi hiyo ilikuwa ya kukarabati maeneo ya Ghaza yaliyoharibiwa vibaya katika vita vya siku 50 ya utawala wa Kizayuni dhidi ya ardhi hiyo ya Palestina mwaka 2014. Vita hivyo vilipelekea watu zaidi ya 2,500 kuuawa shahidi na kuvuruga kabisa uchumi wa eneo hilo.

Tokea mwaka 2007, Israel ikishirikiana na Misri ililiwekea eneo la Ghaza mzingiro wa kuogofya baada Harakati ya Hamas kupata ushindi katika uchaguzi wa kidemokrasia. Shirika la kutoa misaada la Oxfam la Uingereza limesema itachukua miaka 100 kujenga upya Ghaza iwapo mzingiro wa sasa wa Israel utaendelea.